Msanii Moses Bushagama aka Mez B
aliyewahi kung’ara na ngoma ya #KamaVipi aliyompa collabo mwanadada RAY C
na kutesana na nyimbo zake kibao, amefariki dunia muda mfupi uliopita
huko mjini Dodoma nyumbani mama yake mzazi. Taarifa zinasema alikuwa
anaumwa sana ingawa DJChokaMusic haikuweza kujua kwa haraka alikuwa
anasumbuliwa na nini kutokana na mama yake kuonge kwa shida wakati
tukizungumza nae.
Mungu ailaze roho ya marehemu mahala pema peponi! – Taarifa zaidi zitakujia kadri tutakavyozipokea!
HIZI NI BAADHI ZA VIDEO ALIZOKUWA AMEZIFANYA MAREHEMU MEZ B

Post a Comment