OSTAZ JUMA AMUANIKA MKEWE NA MTOTO WAKE

Ostaz Juma (kushoto) akiwa na mkewe Mariamu na mwanae Hayyat
 
Mariamu Daudi
 
Mtoto Hayyan Juma
 
Ostaz Juma Namusoma
 
Ostaz Juma akiwa Cape of Good Hope
Baada ya usiri wa muda mrefu, bosi wa Mtanashati Entertainment, Ostaz Juma Namusoma ameamua kumuweka hadharani mkewe na mototo wake na hivyo kuzima zile tetesi kuwa Ostaz ni msela tu asiye na mke wala mtoto.

Kupitia ukurasa wake wa Facebook, Ostaz Juma ameweka picha ya mkewe ajulikanaye kwa jina la Mariamu Daudi au mama Hayyan akiwa pamoja na mtoto wao wa kiume, Hayyan Juma.
Sambamba na picha hizo, Ostaz alisindikiza na maneno yasemayo:

“For those who didn't know that I have a wife and a kid, let it be known now...kwamba mimi nina mke na mtoto, nampenda sana mke wangu (mary david) na nampenda sana mwanangu hayyan boy hayyan juma. namuomba sana mungu atuhifadhi na maadui wa kibinadamu na wasio jua thamani ya familia ya mtu, eeh mola mjaalie mke wangu maisha marefu na afya na amani ya moyo wake na utulivu, utupe watoto wengine zaidi ya huyu, aamiin, nakupenda sana mke wangu popote utakapo kua ikumbuke familia yako”.

Kuibuka kwa Ostaz kumekuja wakati kukiwa na ukimya kuhusu kampuni yake aliyoianzisha ya kuendeleza vipaji vya wasanii ya Mtanashati Entertainment ambayo miaka miwili iliyopita iliibuka kwa kasi na kumrudisha tena kwenye game msanii  PNC, kuwapa sapoti akina Mkude Simba na marehemu Sharo Milionea.
Akizungumzia ukimya wa Mtanashati, Ostaz alidai kuwa kampuni yake haijafa na haiwezi kufa ila kwa uwezo wa Mungu na kusema kuwa hivi sasa ana dili na wasanii wachanga na soon atafanya surprise kubwa katika tasnia ya Bongo Fleva!

Post a Comment

Previous Post Next Post