MANCHESTER UNITED YAIFUMUA CAMBRIDGE UNITED 3-0 - Ni Juan Mata, Marcos Rojo na James Wilson

Ikicheza kwa tahadhari kubwa, Manchester United ikahakikisha hairudii makosa, ikaitandika Cambridge United 3-0 katika mchezo wa marudiano wa FA Cup uliochezwa Old Trafford.
Ikiwa bado ina kumbukumbu ya kulazimishwa sare na timu ya daraja la chini kwenye mchezo wa kwanza wiki iliyopita, United ikatumia vizuri nafasi zake na kujikuta inakwenda mapumziko ikiwa inaongoza 2-0 kupitia magoli ya Juan Mata na Marcos Rojo.


Kipindi cha pili United ikaongeza bao la tatu lilifungwa na mshambuliaji kinda James Wilson aliyeingia dakika ya 66 kuchukua nafasi ya Van Persie.
Wilson alifunga bao hilo dakika ya 73 baada ya kupokea pasi safi ya Herrera kabla ya kuutulia kwa guu lake la kushoto na kuachia shuti lililokwenda wavuni.

Post a Comment

Previous Post Next Post