Washauriwa kuacha kuosha uke kwa mvuke

Ukiangalia  video hiyo unaweza kabisa kusema ni vyema na wewe (mke) ukapigwe na stimu mambo yaende safi, lakini hapa pana maneno yasome.
WATAALAMU wameingiza maneneo katika kampeni kubwa inayoendeshwa na Gwyneth Paltrow ya kusafisha uke kwa mvuke.
Wataalamu wamesema tabia hiyo inayopigiwa debe na muigizaji huyo si nzuri na kuna hatari ya kuharibu utaratibu wa kawaida wa uke.
Hayo yameandikwa na jarida moja la Marekani.
Katika makala yake imesema kwamba pamoja na  Gwyneth Paltrow kupigia debe shughuli hiyo na kushawishi watu wanaofika Mji wa Los Angeles kuhakikisha wanafika katika kliniki yake na kufanyiwa au kupewa maelekezo ya namna ya kusafisha uke na mvuke.
Muigizaji huyo anasema kwamba tiba yenyewe ni  nyepesi tu kwani unachofanya unakaa kwenye kiti na unaachia mchanganyiko uliomo kwenye mvuke kufanyakazi ya kutakasa sehemu zako za kizazi.
Huduma hiyo ina gharimu dola 50 lakini madaktari waliozungumza na NewsBeat wanasema hawana uhakika na usalama wala faida ya tiba hiyo.
Tikkun Spa wanasema kwamba  huduma hiyo husaidia kutibu hali mbalimbali ikiwamo ya kuhami tumbo la uzazi dhidi ya kansa na majipu.
Pamoja na maelezo hayo, wanaohusika natiba hiyo wanakiri kwamba haijatathminiwa wala kukubaliwa na Mamlaka ya Chakula na Dawa ya Marekani.
Pamoja na ukweli huo, madaktari wanasema kwamba uke umetengenezwa kwa namna ya kwamba unajitunza wenyewe kutokana na majimaji yeye dawa yanayotoka mwilini.
Wataalamu hao wamesema kwamba usafishaji wa uke kwa namna hiyo si lazima utafanya uwe msafi na salama.
"Utoko katika uke si lazima uwe ni dalili mbaya," anasema Dk Suzy Elneil, Mtaalamu wa ushauri wa masuala ya uke wa Hospitali ya Chuo Kikuu  cha London.
"Kuna kauli zinazoamini kwamba utoko huo unaambatana na magonjwa ya zinaa, hii si kweli." alisema na kuongeza kuwa mabadiliko katika utoko uwingi au uchache wake unaweza kuwa ni shida ya homoni  ambayo inaunganishwa kwenye mzunguko wa hedhi wa mwanamke.
Aidha matumizi ya mvuke, sabuni zinazonukia, jeli, dawa za kuua wadudu zinaweza kabisa kubadilisha  afya ya uke na mizania ya  pH.
Madaktari wanasema ni vyema wanawake wakatumia sabuni zisizo na pafyumu kusafishia sehemu ya nje  ya  na ndani ni kazi ya asili kusafisha, uke wenyewe unajisafisha kwa kutumia kemikali mbalimbali zilizopo.
"Siwezi kufikiria kwamba usafishaji wa uke kwa kutumia mvuke (kuflashi kwa maneno mengine) kunasaidia. Kwa kufanya hivyo utaondoa na bakteria muhimu wanahitajika kwa ajili ya kusafisha  na kuuliza uke," anasema Professora Ronnie Lamont wa Royal College of Obstetricians and Gynaecologists.
Wataalamu wamesema matumizi ya mvuke kama ilivyo katika matumizi mengine inaweza kuleta madhara katika uke.

Post a Comment

Previous Post Next Post