Picha za mahaba za Nay Wa Mitego Zasababisha ‘mkewe’ aondoka na mtoto nyumbani

 Zile picha za mahaba za msanii wa Hip Hop Bongo,Nay Wa Mitego akiwa na msichana kitandani zimezua balaa kwa mama mtoto wake Siwema Edson ambaye baada ya kuziona aliamua kumchukua mtoto wake na kuondoka nyumbani kwa msanii huyo maeneo ya Kimara,jijini Dar.
Siwema akizungumza na Soudy Brown kupitia Uheard alisema kuwa alipata mshtuko mkubwa sana baada ya kuziona picha hizo ambapo aliamua kuondoka nyumbani na mtoto wake mdogo.
 ‘’Kiukweli zile picha zilinishtua sana nilimuuliza Nay akaniambia ni video lakini sikumuelewa tuligombana na mimi nikaamua niondoke nyumbani kwani nimeona kama kanidhalilisha,’alisema Siwema.
Hata hivyo Nay akijitetea alisema kuwa zile picha zilivujishwa na mtu ambaye huwa ana post account yake ya Instagram na kwamba ni picha za video yake ya ngoma yake mpya ambayo ataiachia hivi karibuni iitwayo ‘Only You’.

Post a Comment

أحدث أقدم