PICHA:WANAFUNZI WA SHULE YA SEKONDARI ILALA JIJINI DAR ES SALAAM WALIPOANDAMANA KWENDA KWA MKUU WA MKOA WA DAR KUPINGA KUBOMOLEWA UZIO WA SHULE YAO

 Wanafunzi wa shule ya Sekondari Ilala, iliyopo Karakata Jijini Dar es Salaam wakiandamana jana kwenda kwa Mkuu wa Mkoa wa Dar es Salaam kufikisha kilio chao cha kubomolewa uzio wao na wananchi wanaoizunguka shule hiyo.

 wanafunzi hao walisema kuwa kiliochao hasa ni kutokana na uongozi wa shule kuwachangisha shilingi 20,000/= kila mmoja kwaajili ya ujenzi wa uzio huo uliovinjwa juzi jioni baada ya wao kutoka shule. 

Amri ya kubomolewa kwa ukuta huo inadaiwa kutolewa na Mwenyekiti wa Serikali za Mtaa huo, Greyson Maliki kinyume cha sheria  sio cha kiungwana kwani pamoja na kwamba kulikuwa na mgogoro wa muda mrefu katika eneo hilo, bado shule hiyo ina wanafunzi wa eneo hilo na wazazi wao wamelipia katika ujenzi wa ukuta.
  Wanafunzi hao
  Wanafunzi hao wakiandamana na kufunga barabara ya Nyerere, Mandela na Uhuru kwa muda wakati wakipita kwenda Ofisi ya Mkoa wa Mkoa.
 Wanafunzi hao wakiwa katika Ukumbi wa Mikutano Ofisi ya Mkuu wa Mkoa leo. Ambapo hata hivyo, Mkuu wa Mkoa walipishana nae njiani kwani alikwenda shuleni kwao kusikiliza kero yao. 


Mwenyekiti huyo, Afisa Mtendaji wa Kata na Mjumbe wa mtaa huo wameshikiliwa na jeshi la polisi kwa mahojiano.
 Ulinzi mkali ofisi ya Mkuu wa Mkoa.Picha na Father Kidevu Blog

Post a Comment

Previous Post Next Post