
Ikiwa
na nyota wake Cristiano Ronaldo na Gareth Bale, Real Madrid imechukua
kipigo cha aibu 4-0 kutoka kwa watani wao wakubwa Atletico Madrid.
Hii
ni mara ya kwanza ndani ya miaka 64 kwa Real Madrid kufungwa mara tatu
mfululizo kwenye uwanja wa wapinzani wao hao wa jiji la Madrid, lakini
kipigo hiki kilikuwa cha aibu zaidi - klabu hiyo tajiri ilifunikwa
vibaya kuanzia filimbi ya kwanza hadi mwisho wa mchezo.


Washambuliaji
wa Real Madrid wenye thamani ya pauni milioni 250 Bale, Ronaldo na
Karim Benzema walifanikiwa kupiga shuti moja tu katika kipindi cha
kwanza kilichotawaliwa na Atletico Madrid ambao walifunga mara mbili
kupitia kwa Tiago na Saul.

Magoli mengine ya Atletico Madrid katika mchezo huo wa La Liga, yalifungwa na Greizmann na Mandzukic.
Atletico
Madrid (4-4-2): Moya; Juanfran, Miranda, Godin, Siqueira; Tiago, Koke
(Saul 10 [Garcia 71]), Gabi, Turan; Griezmann (Torres 77), Mandzukic.
Post a Comment