Mimba kutunga nje ya mfuko wa uzazi ni tatizo ambalo linaweza
kumpata mwanamke yeyote na linapaswa kufahamika mapema ili hatua muafaka
zichukuliwe.
Kwa kawaida mimba hutunga ndani ya mfuko wa kizazi isipokuwa mara chache huweza kutokea nje ya eneo hili maalumu.
Katika nyumba ya uzazi kuna mirija inayoitwa
fallopian ambayo kazi yake ni kusafirisha mayai kutoka katika kiwanda
chake cha uzalishaji; ovari hadi kwenye mfuko wa uzazi. Hapo ndipo
mimba inapaswa kutokea.
Kwa bahati mbaya ama kutokana na hitilafu fulani
mimba hiyo inaweza ikatungishiwa kwenye moja ya mirija miwili ya kizazi;
upande wa kulia au kushoto.
Ikitokea hivyo, basi itafahamika kuwa mimba hiyo
imetungwa nje ya kizazi. Vilevile mimba inaweza ikawa imetungwa nje ya
nyumba ya uzazi au mirija. Asilimia 95 ya mimba zinazotungwa nje ya
uterasi ama nyumba ya uzazi hutokea kwenye mirija hii ya fallopian.
Mimba zinazotungwa kwenye fallopian husababisha
misuli inayozunguka mirija hiyo kushindwa kufanya kazi kutokana na
mgandamizo wa mimba inavyokua. Hii husababisha mishipa inayopita karibu
na fallopian kupasuka na damu kutoka kwa wingi hali ambayo
isiposhughulikiwa mapema inasababisha madhara zaidi na hata kifo kwa
mama.
Chanzo cha tatizo
Chanzo cha bado hakijajulikana, hata hivyo kuna
vihatarishi ambavyo humfanya mwanamke kuwa katika mazingira ya kupata
tatizo hili,.
Viashiria hivyo ni pamoja na magonjwa kama maambukizi katika mfumo wa uzazi hasa yale yanayosababisha uvimbe.
Vihatarishi vingine ni kama vile matumizi ya vitanzi vya kuzuia mimba au kuoteana kwa tishu za kwenye nyumba ya uzazi.
Mambo mengine yanayoweza kusababisha mimba
kutungwa nje ya nyumba ya uzazi ni uvutaji wa sigara. Nikotini iliyoko
ndani ya tumbaku huchochea kusinyaa kwa mirija ya ya fallopian na hata
kusababisha mirija hiyo kuziba.
Jambo jingine ni upasuaji wa tumbo uliofanyika zamani unaohusu mirija ya fallopian na kusababisha mrija husika kusinyaa.
Post a Comment