Umoja wa mataifa imezituhumu serikali za Tanzania na Burundi kuhusiana na hali katika Jamhuri ya Kidemokrasi ya Congo.
Ripoti
mpya ya kundi la wataalamu wa umoja huo kuhusu Congo, imeituhumu
Tanzania kwa kuwaruhusu viongozi wa kundi la waasi wa FDLR kuandaa
mikutano nchini humo.
Imeeleza pia kwamba wanajeshi wa Burundi wametekeleza unyanyasaji wa kingono.
Taarifa
hiyo ya Umoja wa mataifa inasema kuwa tangu mwaka wa 2013, viongozi wa
FDLR na baadhi ya washirika wao wa kisiasa kutoka Ulaya wamekuwa
wakikutana nchini Tanzania.
Lakini wachunguzi wa Umoja wa
mataifa walipoiuliza serikali ya Tanzania kujibu madai haya ilikanusha
kabisa kuwahi kuakaribisha mikutano yoyote ya waasi ndani ya ardhi yake
na kuongeza kuwa hakujawahi kuwa na mazungumzo yoyote kati ya majeshi
yake na wapiganaji wa FDLR.
Umoja wamataifa umesema pia kuwa una
ushahidi wa pesa zilizotumwa kutoka taifa hilo la Afrika Mashariki kwa
baadhi ya washukiwa nchini Jamhuri ya kidemokrasia ya Congo.
Ripoti
hiyo pia imelaumu kundi hilo la FDLR kwa kutotekeleza ahadi yao ya
kusalimisha silaha na kujisalimisha kufikia Januari mwaka huu.
UN
inasema kuwa FDLR wamewatuma wazee waliodhoofika kiafya pekee
kujisalimisha na kukabidhi silaha chache sana ambazo zina hitilafu.
Kundi
la FDLR, liliundwa mwaka wa 2000 na wahutu waliokimbilia Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo kufuatia mauaji ya kimbari ya Rwanda.
Kundi hilo linapinga utawala wa kitutsi na ushawishi wake katika eneo la maziwa makuu.
Rwanda
imekuwa ikitazama kundi hilo kama tisho kubwa kwa utawala uliopo na kwa
kauli moja na Umoja wa mataifa imekuwa ikishinikiza kupokonywa silaha
kwa wapiganaji wake.
Ripoti hiyo pia imetoa madai ya ubakaji na unyanyasaji wa kimapenzi unaofanywa na wanajeshi wa Burundi katika Kivu ya Kusini .
Wataalamu
hao wa Umoja wa mataifa wamependekeza serikali za Burundi na Jamhuri ya
Kidemokrasia ya Congo zifanyie uchunguzi madai hayo ambayo wanasisitiza
yalifanywa namajeshiya Burundi pamoja na kikundi cha vijana wapiganaji
wajulikanao kama Imbonerakure.(BBC)
إرسال تعليق