Hali
hiyo ilijitokeza wakati wa Mkutano wa Bunge wa 18 ukihitimishwa
mwishoni mwa wiki na kubakia miwili tu Bunge la 10 kufikia tamati, hivyo
kwa kila hali uchaguzi mkuu kuzidi kunukia na kazi kubwa ikiwa ni
kupatikana kwa rais wa tano wa Tanzania.
Kwa
kitambo sasa kumekuwa na makundi yanayosigana kila moja likiwa na
mgombea wake, hata hivyo mpambano mkubwa wa kumpata mgombea unaonekana
kuwa zaidi ndani ya Chama Cha Mapinduzi (CCM), kurithi mikoba ya Rais
Jakaya Kikwete, anayehitimisha uongozi wake wa utawala Oktoba mwaka huu
kwa mujibu wa katiba ya Jamhuri ya Muungano wa Tanzania.
Katika
mbio hizo, sasa ni rasmi kwamba kundi la wabunge wanaodaiwa kufikia 150
walikutana katika chakula cha jioni mjini Dodoma eneo la Kilimani
mwishoni wiki iliyopita. Wote waliopata fursa ya kuzungumza katika hafla
hiyo, walisema wazi kuwa wanamuunga mkono Lowassa katika mbio za urais.
Lowassa
ambaye pia ni mbunge wa Monduli na Waziri Mkuu wa zamani, anadaiwa
kutakiwa na wabunge hao kuwa muda ukifika achukue fomu za kuwania urais
kwa tiketi ya CCM katika uchaguzi mkuu utakaofanyika Oktoba mwaka huu.
Ingawa
kumekuwa na tetesi na minong’ono ya Lowassa kuungwa mkono ndani ya CCM
kuwania nafasi hiyo ya juu kabisa ambayo pia itampa fursa ya kuwa
Mwenyekiti wa chama hicho, uamuzi wa wiki iliyopita wa wabunge hao
kusimama hadharani unaibua moto mkubwa wa kinyang’anyoro cha urais huku
jina la Lowassa likizidi kutajwa kama chaguo la wengi.
Habari
ambazo Mpekuzi imezipata zinasema kuwa wengi wa wabunge waliozungumza
walitaja sifa za kuwania urais, wakisisitiza kuwa Lowassa anazo na
kwamba ni mtu pekee kwa sasa wanaoona kuwa CCM inaweza kuingia kwenye
uchaguzi ikiwa na uhakika wa ushindi kama ataipeperusha bendera ya chama
hicho.
Katika
hafla hiyo ambayo pia Lowassa anadaiwa kuhudhuria, mbunge mmoja mkongwe
mkoani Kagera (CCM), anadaiwa kusema kuwa wabunge marafiki wa Lowassa
wanamuomba agombee kutokana na kuwa na sifa zote za uongozi hasa katika
zama za sasa ambazo taifa linahitaji mtu wa kulikwamua.
"Mimi
as a senior citizen (kama raia mkongwe), huu ni mwaka muhimu, Oktoba
tutakuwa na uchaguzi mkuu wa kumchagua kiongozi atakayeisukuma mbele
nchi yetu… sote tunafahamu chama chetu bado hakijatangaza taratibu,
lakini sisi wabunge marafiki zako tunakuomba, muda ukifika chukua fomu
kwa sababu unatosha," vyanzo vyetu vilimnuku mbunge huyo akimshawishi Lowassa katika hafla hiyo.
Mbunge
huyo anadaiwa kuainisha sifa muhimu za kiongozi kuwa ni mwenye elimu
madhubuti, uwezo wa kuona mbali (vision), muwajibikaji na mchapakazi,
uwezo wa kutenda na tabia nzuri, vitu ambavyo alisema kuwa Lowassa
anavyo hasa akirejea rekodi yake ya uwaziri mkuu kati ya 2005 hadi
Februari 2008.
"Kule
kwangu wananiuliza yule waziri mkuu aliyeleta hizi shule za kata yuko
wapi? Mimi nawajibu atarudi tu. Na kila mtu mitaani anataja jina lako
kwa hiyo sauti ya watu (wengi) ni sauti ya Mungu," alisema mbunge huyo.
Wabunge
wengine ambao walipata fursa ya kuzungumza ni pamoja na Viti Maalum
(Singida), Diana Chilolo, mbunge shabiki wa klabu ya Simba atokaye mkoa
wa Tanga(CCM), Mary Chatanda wa Viti Maalum (CCM) na mbunge kutoka
Ruvuma ambaye ni kada muhimu wa kuipigia debe CCM katika kila kipindi
cha uchaguzi.
Chilolo
anadaiwa kuungana na mbunge mkongwe kutoka Kagera, akisema kuwa Lowassa
ni chaguo la wengi, huku mbunge kutoka Tanga akinukuliwa akisema kuwa
Lowassa ni binadamu mwenye imani na upendo wa hali ya juu.
"Huyu
mzee mbali ya uwezo mkubwa wa kufanya kazi, lakini ana huruma... mimi
niko tayari kufukuzwa CCM kwa kumuunga mkono Lowassa,” alisema mbunge kutoka Tanga.
Pia
mbunge huyo (kutoka Tanga), anadaiwa kuahidi kuwa atatumia nafasi yake
kuhakikisha kwamba watu wote wanamuunga mkono Lowassa.
Mbunge huyo wa Tanga anadaiwa kusema kuwa kwa kumuona Chatanda katika hafla hiyo, kunadhihirisha kukubalika kwa Lowassa.
Chatanda
ambaye pia ni Katibu wa CCM Mkoa wa Singida, inaaminika kuwa alikuwa
hasimu mkubwa wa Lowassa wakati akiwa katibu wa chama tawala mkoa wa
Arusha.
Habari
zinasema kuwa Chatanda na Lowassa walikuwa na uhasama mkubwa na wote
waliokuwa wanamuunga mkono Lowassa mkoani Arusha walionja makali ya
Chatanda.
Vyanzo
vya habari vilivyojipenyeza kwenye hafla hiyo iliyofanyika baada ya
iliyokuwa imeandaliwa na Waziri Mkuu, Mizengo Pinda, vinasema kuwa
Chatanda mwenyewe aliposimama kuzungumza alikiri kuwa alikuwa hamuungi
mkono Lowassa pamoja na kwamba wanafahamiana kwa muda mrefu, lakini sasa
anaungana na wale wanaomuomba agombee.
"Mimi
na Edward hatuna ugomvi, wapambe wake ndiyo walikuwa wanatuchonganisha,
na kwa kweli sikuwa kabisa namuunga mkono, lakini wagombanao ndiyo
wapatanao…mimi sasa hivi nimeingia mwili mzima kumuunga mkono Edward na
hakuna wa kunitoa," chanzo chetu kinamnukuu Chatanda, akitangaza msimamo mpya wa kisiasa katika makundi ya kusaka urais kupitia CCM.
Kutokana na msimamo huo mpya, habari zinasema kuwa Chatanda alipigiwa makofi na wabunge wenzake.
Naye
mbunge kutoka Ruvuma ambaye alishatangaza siku nyingi kuwa anamuunga
mkono Lowassa katika safari yake kuelekea Ikulu, anadaiwa kusema kuwa
ushahidi wa kukubalika kwa Lowassa ulidhihirika wakati wa kilele cha
sherehe za miaka 38 ya CCM mjini Songea Februari Mosi mwaka huu,
kutokana na kushangiliwa na uwanja mzima mara alipowasili.
"Sikilizeni
niwaambie... miye nilikuwapo uwanjani, wale wengine wote
hawakushangiliwa pamoja na kutembea mbali na jukwaa ili watu wawaone.
Lakini huyu Lowassa alivyoteremka mbele tu ya jukwaa kuu, uwanja mzima
ulilipuka," vyanzo vyetu vilimnukuu mbunge huyo akisema kwenye hafla hiyo.
Naye
mbunge wa jimbo mojawapo linaloaminika kuwa ni ngome ya CCM jijini Dar
es Salaam ananukuliwa akimuelezea Lowassa kama kiongozi shupavu na
makini.
"Uwezo wake naujua... kwa kweli tunajifundisha mengi kutoka kwake," alisema mbunge huyo.
Naye
mbunge kutoka Zanzibar (CCM), anayesifika kwa kuwa mkali kila mara
linapofikia suala la kutetea maslahi ya visiwa hivyo, ananukuliwa
akimuomba Lowassa kukubali ombi lao kwani anatosha kwenye kiti cha
urais.
Habari za ndani zinasema kuwa Lowassa ambaye hata hivyo hajatangaza rasmi nia ya kuwania urais, aliposimama kujibu kauli za wabunge hao, anadaiwa kusema suala la urais ni jambo zito hivyo kwa sasa anamwachia kwanza Mungu.
"Ndugu
zangu nafarijika sana kwa kauli zenu, lakini hili suala la urais ni
kubwa, tumuachie huyu aliye juu (Mungu), yeye akiamua liwe linakuwa," vyanzo vyetu vilimnukuu Lowassa akisema wakati wa hafla hiyo.
إرسال تعليق