
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima
Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani ya Nchi, Pereira Ame Silima alieleza
bungeni jana kuwa wafungwa hao walirejeshwa kutumikia adhabu zao
nchini, kufuatia Tanzania kuingia mikataba ya kubadilishana wafungwa na
nchi hizo mbili.
Awali Ritha Kabati (Viti Maalum - CCM) alitaka kufahamishwa ni nchi
ngapi ambazo Tanzania ina utaratibu wa kubadilishana wafungwa na ikiwa
mataifa hayo yapo ni wafungwa wangapi wamerejeshwa nchini kupitia mpango
huo.
Katika swali lake la nyongeza, Kabati alihoji sababu zinazozuia
Tanzania kuanzisha uhusiano kama huo na India na China, kutokana na
uwepo wa raia wake wengi wanaotumikia vifungo kwa sababu mbalimbali,
zikiwamo biashara ya mihadarati.
Naibu Waziri Silima alisema, uhusiano wa China, India na Tanzania
ni mzuri lakini ni katika mataifa ambayo raia wa Tanzania wamefanya
makosa ya kisheria na kwa Afrika ni Kenya.
Alisema kupitia njia za diplomasia, wanaendelea kufanya taratibu za
kuingia mikataba na nchi hizo, ili kufanikisha uwezekano wa kuwaruhusu
wafungwa hao, kurejeshwa nchini ili kutumikia adhabu zao kwa muda
utakaokuwa umebakia baada ya kusainiwa mikataba ya mahusiano ya
kubadilishana wafungwa.
“Watu ambao wako nchi mbalimbali wanapowasiliana na balozi zetu
zilizo kwenye nchi husika, wanapata misaada ya kisheria na hatuwezi
kuwatelekeza isipokuwa tunatoa wito kwa wananchi wanapotaka kwenda nchi
yoyote ile, kwanza wajifunze sheria za mataifa hayo” alieleza.
Waziri Silima alikanusha taarifa kwamba serikali imeingia mikataba
ya aina hiyo na nchi hizo mbili kwasababu wafungwa wengi waliyokuwa huko
ni waliyokuwa wakitumikia adhabu ya kifungo kwa kutiwa hatiani kuhusika
na biashara haramu ya mihadarati.
Alisema hata katika nchi ambazo Tanzania haijafanikiwa kuwa na
mikataba ya kubadilishana wafungwa, makosa mengi makubwa wanayokabiliwa
nayo wafungwa husika ni biashara haramu ya mihadarati na kwamba jambo la
msingi ni kuwapa malezi bora vijana, ili kuwaepusha na kuingia kwenye
janga la biashara za madawa hayo ya kulevya.
إرسال تعليق