Wananchi longido walalamikia watendaji kukwamisha miradi

Wananchi wa wilaya ya longido mkoani arusha wamesema   hatua ya serikali ya kutenga fedha za miradi ya maji  na watendaji kushindwa kuzifikisha kwenye miradi  husika  ni matumizi mabaya ya kodi zao kwani uzoefu unaonyesha kuwa miradi yote inayoanzishwa  na  kukwama  inakufa  kabisa  na gharama  zote   za  awali  zinakuwa za  bure.
Wananchi hao wametoa mfano wa mradi wao wa maji ambao  ni miongoni mwa ilikwama kwa sababu za kuchelewa kwa  fedha na wamesema   wameanza  kukata tamaa   kwani   baadhi ya miundombinu imeanza kuharibika maelezo ambayo  yamethibitishwa  na  baadhi ya viongozi akiwemo  mwenyekiti wa  halmashauri  hiyo.
Kufuatia malalamiko ya wananchi hao naibu waziri wa  maji Bw,Amosi Makala ametembelea na kujionea mradi huo   na amewahakikishia kuwa serikali itamalizia fedha  zilizobaki na mradi utakamilishwa haraka  iwezekanavyo.
Malalamiko ya kuwepo kwa miradi mingi inayoanzishwa  na  kukwama kutokana na kuchelewa ama kukosekana kwa fedha  yamekuwa yakitolewa na wananchi wa maeneo mbalimbali  jambo linalodaiwa kuchangiwa na urasimu.

Post a Comment

Previous Post Next Post