Wananchi wa wilaya ya longido mkoani
arusha wamesema hatua ya serikali ya kutenga fedha za miradi ya maji
na watendaji kushindwa kuzifikisha kwenye miradi husika ni matumizi
mabaya ya kodi zao kwani uzoefu unaonyesha kuwa miradi yote
inayoanzishwa na kukwama inakufa kabisa na gharama zote za
awali zinakuwa za bure.
Wananchi hao wametoa mfano wa mradi wao wa maji ambao ni miongoni
mwa ilikwama kwa sababu za kuchelewa kwa fedha na wamesema wameanza
kukata tamaa kwani baadhi ya miundombinu imeanza kuharibika maelezo
ambayo yamethibitishwa na baadhi ya viongozi akiwemo mwenyekiti wa
halmashauri hiyo.
Kufuatia malalamiko ya wananchi hao naibu waziri wa maji Bw,Amosi
Makala ametembelea na kujionea mradi huo na amewahakikishia kuwa
serikali itamalizia fedha zilizobaki na mradi utakamilishwa haraka
iwezekanavyo.
Malalamiko ya kuwepo kwa miradi mingi inayoanzishwa na kukwama
kutokana na kuchelewa ama kukosekana kwa fedha yamekuwa yakitolewa na
wananchi wa maeneo mbalimbali jambo linalodaiwa kuchangiwa na urasimu.
إرسال تعليق