NI shida! Wakazi wa Mlandizi mkoani Pwani mwishoni mwa wiki iliyopita
walijikuta wakishinda nje ya nyumba moja ya kulala wageni iitwayo
Kilimahewa Guest House baada ya kuwepo taarifa za watu wawili, mtu na
mpenzi wake kunatana baada ya kudaiwa kufanya mapenzi majira ya asubuhi.
Mwananchi akitumia tochi kuwasaka uvunguni.
Kwa mujibu wa mashuhuda wa tukio hilo, taarifa za kuwepo kwa tukio
hilo zilisambaa kwa kasi na chanzo chake kinadaiwa ni mwendesha pikipiki
mmoja aliyetoa habari hizo.
Kutokana na uvumi huo, mamia ya watu walijazana nje ya nyumba hiyo,
huku wakisisitiza kutaka kuwaona watu hao.“Saa 3 asubuhi kuna mtu mmoja
wa pikipiki alikuja akatuambia kuwa watu wamenasiana katika Gesti ya
Kilimahewa, huwezi amini watu wametoka Chalinze kwa ajili ya tukio hili
na sisi harakaharaka tukafika hapa kuona nini kinaendelea, mpaka sasa
hatujui kama ni kweli ama sio kweli.
“Polisi wamefika hapa wamesema hakuna ukweli baada ya kuikagua gesti
nzima lakini hata hatuamini tupotupo tu,” walisema baadhi ya akina mama
waliokuwa nje ya gesti hiyo, waliodai wametokea Chalinze.
Diwani wa Kata ya Janga (CCM), Mlandizi, Fedilia Swai alifika eneo la
tukio baada ya kupokea taarifa na kukagua kila chumba na aliwaambia
wananchi kuwa hakuona chochote ndani ya gesti hiyo na kwamba huo ni
uvumi ambao hauna ukweli wowote na kuwataka watu warudi makwao.
Muonekano wa kitanda walichokuwa wakitumia wapenzi hao.
“Unajua muda huu nilikuwa katika shughuli nyingine, lakini ilinibidi
nifike hapa baada ya kupata taarifa kuwa kuna wananchi wangu
wamenasiana. Nimeingia vyumba vyote hakuna kitu kama hicho nimeingia na
mashahidi wawili, mwanaume mmoja na mwanamke mmoja tumekagua kote hakuna
watu hao.
Nasisitika hizi taarifa ni za uongo tena uzushi mkubwa.”
Nasisitika hizi taarifa ni za uongo tena uzushi mkubwa.”
Kauli ya diwani huyo haikutosha mpaka pale alipokuja tena mwenyekiti
wa eneo hilo kwa tiketi ya Chama cha Wananchi (CUF), Kilindo Ahmed
ambaye pia alitoa kauli kama hiyo na kuwataka wananchi hao kuteua
wawakilishi wawili kwa ajili ya kwenda kuthibitisha ndani ya nyumba
hiyo.
Pamoja na mashahidi hao kueleza ukweli wa kutokuwepo kwa tukio hilo, bado wananchi hawakuamini.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdallah Saidi alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma ili akose wateja katika biashara yake.
Kwa upande wake, mmiliki wa nyumba hiyo, Abdallah Saidi alikanusha taarifa hizo na kusema kuwa amefanyiwa hujuma ili akose wateja katika biashara yake.
...Wananchi wakisubiria kwa nje.
“Kuna watu wamesambaza uvumi huu makusudi ili kuniharibia biashara
yangu, huu ni mpango wa kunichafua kibiashara, angalia siku nzima
sijafanya kazi yoyote, wateja wangu wataanza kuogopa kuja,” alilalama
mmiliki huyo.
إرسال تعليق