MSANII mkongwe katika
gemu la filamu Bongo, Wastara Juma ameapa kumshtaki mtu atakayekamata
kutokana na baadhi ya mashabiki kuwa na tabia ya kumtukana matusi ya
nguoni mtandaoni huku wakimhusisha na marehemu mumewe, Sajuki.
Msanii mkongwe katika gemu la filamu Bongo, Wastara Juma.

Akizungumza na gazeti hili, Wastara alisema anajisikia vibaya baadhi
ya mashabiki wanavyomtukana kwenye mitandao ya kijamii jambo ambalo siyo
zuri kwani wanaingilia maisha yake binafsi na kibaya zaidi wanamhusisha
Sajuki.
“Ukweli sipendi kabisa na nitamshtaki mtu maana wananitengenezea
chuki kwani wakati mwingine wananitukana, wanamtukana sana Bondi huku
wakidai kwamba nilikuwa naomba Sajuki afe ndiyo nifanye mabaya sasa
sijui nimefanya kitu gani kibaya, kuwa na Bondi nimekuwa naye baada ya
mume wangu kufariki maana mimi ni binadamu na kama angekuwepo
nisingekuwa na mwanaume mwingine zaidi yake,” alisema Wastara.
إرسال تعليق