Watoto 320 kutotka familia maskini za
jamii za wafugaji mkoani arusha wamepata ufadhili wa masomo kuanzia
chekechea hadi sekondari kutoka nchi za ulaya hatua inayolenga
kupunguza matatizo yanayowakabili wananchi wengi wa jamii hizo
yanayochangiwa na ukosefu wa elimu.
Wakizungumza wakati wa uzinduzi wa majengo ya shule ya sekondari ya
Olosiva iliyoko wilayani arumeru wanakosoma watoto hao baadhi ya
wafadhili wa watoto hao kutoka Denmark na Finland wamesema pamoja na
hatua hiyo ushirikiano wa dhati wa kuzisaidia jamii za wafugaji
kielimu unahitajika vinginevyo misaada itaendelea kutolewa na umaskini
utaendelea kuwakabili.
Mratibu wa mfuko wa kuwsaidia watoto hao hapa nchini Dr.Edwin Falc
amesema kimsingi umaskini unazikabili jamii za wafugaji haupaswi
kuwepo kulingana na rasilimali zinazowazunguka jambo linaloonyesha wazi
kuwa lipo tatizo lingine linalohitaji kupewa kipaumbelea ambalo ni
elimu.
Mwenyekiti wa kitongoji cha Olosiva Bw,Samson Sabaya amesema
utaratibu wa wahisani hao wa kuwekeza katika elimu na kupeleka misaada
moja kwa moja kwa walengwa unafaa kuigwa na wadau wengine kwani
unaepusha tatizo.

إرسال تعليق