Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene akifungua mkutano kwa ajili ya kujadili nishati endelevu nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable Energy for All) ulioshirikisha sekta binfasi, wataamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini. Mkutano huo uliofanyika katika hoteli ya Protea jijini Dar es Salaam lengo lake lilikuwa ni kubadilishana uzoefu kwa ajili ya kuboresha sekta ya umeme nchini.
Meneja Hifadhi kutoka Shirika la WWF Nchini Dk. Amani Ngusaru akitoa hotuba ya kumkaribisha Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene (hayupo pichani)
Sehemu ya wadau wa mkutano kwa ajili ya kujadili nishati endelevu nchini kwa wote ( Tanzania Sustainable Energy for All) ulioshirikisha sekta binfasi, wataamu kutoka Wizara ya Nishati na Madini pamoja na wadau wa nishati nchini wakifuatilia kwa makini hotuba iliyokuwa inatolewa na Waziri wa Nishati na Madini George Simbachawene ( hayupo pichani)
إرسال تعليق