10 QUESTIONS VAI WA UKWELI AFUNGUKIA ISHU YA USAGAJI, KUTOA MIMBA!

Wiki hii tunaye msanii wa filamu anayefahamika sana kwa jina la Vai wa Ukweli lakini jina lake halisi ni Isabela Fransis. Mwandishi wetu Hamida Hassan alimbana kwa maswali 10 na yeye alitoa ushirikiano katika kuyajibu, shuka naye…
Ijumaa: Hebu waambie wasomaji kuhusu maisha yako ya kimapenzi maana wengi wanahisi hujatulia na una wanaume kibao.

Isabela Francis ‘Vai wa Ukweli’ akiwa katika ofisi za GPL.
Vai: Ukweli ni kwamba ninaye mpenzi wangu ambaye anaitwa Bon, tunapendana sana na tuna mipango ya kujenga familia yetu. Mimi siyo machepele kama wanavyofikiria.
Ijumaa: Inadaiwa unaishi kinyumba na mwanaume huyo, je familia yako inalichukuliaje hilo?
Vai: Mama yangu anajua mimi nakaa kwa rafiki yangu kwa hiyo hawezi kunifikiria tofauti sana ila muda ukifika atajua tu.
Ijumaa: Unapokuwa na mpenzi wako unapenda kuvaa mavazi gani?
Vai: Mavazi tena? Yani niwe na mpenzi wangu chumbani halafu nivae nguo! Kimsingi sivai chochote.
Ijumaa: Baadhi ya waigizaji wanagandwa na skendo ya kujiuza ili kujiongezea kipato, hivi wewe ukiacha usanii unafanya kazi gani nyingine?
Vai: Mbali na uigizaji pia nafanya biashara mbalimbali, nina mgahawa na pia nakodisha mikanda ya filamu.
Ijumaa: Marafiki zako wengi wanaonekana ni micharuko, hivi ulishawahi kufanya usagaji kwa namna yoyote ile?
Vai: Huo uchafu sijawahi kuufanya, madhara yake ni makubwa sana. Hao marafiki unaosema ni micharuko siwezi kuwazungumzia.
Ijumaa: Vipi hili la kutoa mimba? Maana inasemekena umeshawahi kufanya hivyo.
Vai: Kiukweli napenda sana kupata mtoto lakini sijawahi kupata mimba sijui kwa nini.
Ijumaa: Mabinti wengi wa mjini kuvaa ‘kufuli’ kwao ni mwiko, kwako hili likoje?
Vai: Hata mimi ni mmoja wao kwa sababu zinaniwasha ndiyo maana sipendi kuvaa.
Ijumaa: Kuna hii tabia ya baadhi ya wasanii kupora mabwana wa mwenzao, wewe ilishawahi kukutokea?
Vai: Mimi sijawahi kumpora bwana wa mtu ila hiyo tabia ipo lakini wa kwangu namlinda asije akaniponyoka.
Ijumaa: Kuna picha zako f’lani za utupu ziliwahi kuvuja, hivi ilikuwaje?
Vai: Hayo ni mambo yaliyopita ambayo sitaki hata kuyakumbuka.
Ijumaa: Uliwahi kunaswa kwenye ule mtego wa wasanii kujiuza, kwani huwa unachepuka?
Vai: Siyo kwamba nilinaswa ila nilikuwa naujua mchezo mzima, nilitaka kujua mwisho wa yule aliyekuwa ananitaka wakati hatujuani utakuwaje.

Post a Comment

أحدث أقدم