Aibu iliyoje! Tukio la aina yake limetokea maeneo ya Diluxe jijini
hapa baada ya mama mmoja aliyejitambulisha kwa jina la Faudhia almaarufu
mama Baraka kumfumania mumewe akisaliti ndoa yao mbichi.
Faudhia akihamaki baada ya kufumaniwa.
Kwa mujibu wa mama Baraka, amekuwa akimfuatilia mumewe kwa muda mrefu
baada ya kutonywa na wambeya kuwa baba mtoto wake huyo amekuwa
akichepuka na ‘kichenchede’ (mrembo) wa mjini.
Siku ya tukio, hivi karibuni ilidaiwa kwamba mume huyo alirudi
nyumbani mapema, akapumzika kidogo, majira ya saa sita mchana aliamka,
akaoga na kupewa chakula kama kawaida kisha akamuaga mkewe kuwa anaenda
ofisini kuna dharura imetokea ghafla.
Kwa mujibu wa mke huyo, jamaa alipotoka tu naye akachukua pikipiki
ambayo ilikuwa tayari imeandaliwa na kuanza kumfuatilia kwa nyuma kila
alipokuwa anaenda ambapo alienda katika baa mbalimbali za Villa Park
Resort, Kibo na nyingine.
Ilisemekana kwamba, alipofika Diluxe Night Club, alipiga honi kisha
akajitokeza kimwana mmoja na kuingia kwenye gari hilo wakaondoka,
walipofika kwenye eneo la giza maeneo hayohayo ya Diluxe Night Club,
gari lilisimama, wakashuka, wakahamia siti ya nyuma.
Kamanda wa Oparesheni Fichua Maovu (OFM) ya Global Publishers na vijana wake, wakiwa katika pikipiki zao ziendazo kasi wakisakanya habari maeneo ya Jiji la Mwanza ghafla walipokea taarifa kutoka kwa chanzo chao kuwa kuna tukio maeneo hayo.
OFM walifika maeneo hayo na kukuta timbwili la nguvu ndani ya gari
huku mama mmoja aliyevaa kininja akimwadhibu msichana aliyekuwa nusu
utupu na mumewe ndani ya gari.Wakati wa timbwili hilo, mchepuko alivaa
suruali na kusahau kuvaa kufuli pakaendelea kuchimbika.
MAMA BARAKA AFUNGUKA
Akizungumza na OFM akiwa eneo la tukio, mama Baraka alisema kuwa alikuwa na kazi kubwa ya kumfuatilia mumewe kwa siku nyingi lakini mumewe huyo alikuwa akipiga chenga.“Nilianza kumfuatilia mume wangu kwa muda mrefu sana baada ya kupata taarifa kuwa huwa ana tabia ya kufanya mapenzi kwenye gari na wanawake.“Nilishamuuliza zaidi ya mara tatu kutaka kujua kama kweli ana tabia hiyo lakini alinikatalia katakata.”

MUME ATAKA KUKATA MSHIKO
Mume huyo alipoulizwa juu ya tabia hiyo alikataa katakata kuongea na kuwambia makamanda wa OFM kuwa hayo mambo anaomba yaishie hapohapo kisha kuzama kwenye waleti na kutoa fedha.
Mume huyo alipoulizwa juu ya tabia hiyo alikataa katakata kuongea na kuwambia makamanda wa OFM kuwa hayo mambo anaomba yaishie hapohapo kisha kuzama kwenye waleti na kutoa fedha.
Hata hivyo, makamanda wetu walizikataa na kuendelea kufanya kazi yao
kwa mujibu wa kiapo chao cha kutopokea hongo wala rushwa hivyo
waliondoka eneo hilo wakimwacha mama Baraka akipambana na mumewe huku
binti akiachiwa aende zake.
إرسال تعليق