Baada ya mahojiano, Gwajima Aachiwa kwa Dhamana

Askofu wa Kanisa la Ufufuo na Uzima Josephat Gwajima (pichani) leo  ameachiwa  kwa  dhamana  baada  ya  kutolewa  hospitali  ya  TMJ  alikokuwa  amelazwa  baada  ya  kupoteza  fahamu  na  kisha  kupelekwa  kituo  cha  Polisi  oysterbay  kwa  ajili  ya  mahojiano.

Akiongea na waandishi wa habari  mara baada ya kuhojiwa na Jeshi la Polisi  na kupewa dhamana, Gwajima amesema hawezi kutishika  na vikwazo anavyowekewa na Serikali juu ya kuwatetea  wakristo nchini .
 
“Nimetoka kwa amani, nashukuru sana Mungu ameniponya,ila nasema sitoacha kusema ukweli juu ya wakristo wenzangu ambao wanakandamizwa na mifumo ya Katiba ambayo inaonekana wazi”Amesema Askofu Gwajima.
 
Askofu Gwajima amewataka  viongozi wenzake kuheshimu tamko  lililotolewa  na  Jukwaa la Kikristo  Tanzania.
 
“Nawaamomba viongozi wa dini wenzangu tuliheshimu Tamko hili la kikristo na endapo  tutakuwa tofauti basi tutakuwa  tunapingana  na  msimamo wetu  na mimi mwenyewe nawahakikishia nitalitetea mpaka mwisho” ameongeza Gwajima.
 
Alipoulizwa na waandishi wa Habari kuhusu Afya yake Gwajima  amesema hawezi kuzungumzia Afya yake kwa  sasa.
 
Kabla ya kulazwa katika Hospitali ya TMJ, Askofu Gwajima alipelekwa katika Hospitali ya Polisi Kurasini na baadaye Hospitali ya Taifa Muhimbili (MNH) ambapo yeye na wafuasi wake waligoma na kutaka atibiwe TMJ ambapo kuna daktari wake maalumu.

Post a Comment

Previous Post Next Post