Mgombea
wa upinzani nchini Nigeria Muhammadu Buhari ameibuka mshindi wa kiti
cha urais dhidi ya Rais Goodluck Jonathan katika uchaguzi uliofanyika
Jumapili nchini humo.
Kwa
mujibu wa Reuters, Buhari wa chama cha upinzani cha APC amepata kura
million 15.4 dhidi ya kura million 13.3 alizopata Jonathan.
Chama
cha Rais Jonathan All Progressives Congress (APC) kimesema kuwa
Jonathan amekubali matokeo na amempigia simu Buhari kumpongeza kwa
ushindi huo.
Ushindi
huu wa Buhari ambaye ni kiongozi wa zamani wa jeshi unaandika historia
katika taifa hilo kwa kuwa ni mara ya Kwanza kwa chama cha upinzani
kushinda kiti cha urais kwa njia ya kidemokrasia
Baadhi
ya waangalizi wa uchaguzi huo wamepongeza namna uchaguzi ulivyoendeshwa
licha ya kuripotiwa kwa hujuma katika baadhi ya maeneo ambazo
zilisababisha hofu ya kutokea kwa vurugu.
Je, Tanzania tunapoelekea katika uchaguzi mkuu Oktoba 2015 tujifunze nini kutoka katika uchaguzi huu?
Post a Comment