BAADA
 ya mwili wa aliyekuwa Mbunge wa Mbinga Magharibi, Kapteni John Komba 
kuagwa na kusafirishwa kwenda kuzikwa mkoani kwao Ruvuma, msanii wa 
muziki wa dansi, Ramadhan Masanja ‘Banza Stone’ amejikuta akilia na 
kusema ameumia sana kwa kushindwa kwenda kumuaga bosi wake huyo wa 
zamani kutokana na afya yake kuwa si shwari.
Mwanamuziki Ramadhani Masanja ‘Banza Stone’.
Akipiga stori na gazeti hili, Banza alisema amehuzunika sana 
kushindwa kwenda kuuaga mwili wa Kapteni Komba kwani enzi za uhai wake 
alifanya naye kazi ya muziki kwenye Bendi ya TOT lakini kutokana na afya
 kuwa mgogoro alishindwa kabisa.
“Imeniuma sana kushindwa kumzika baba yangu Komba maana nilikuwa 
natamani sana nikamuage mara ya mwisho lakini nikashindwa kutokana na 
afya yangu kuwa mbaya, Komba nilifanya naye kazi sana na kifo chake 
kimeniuma mno,” alisema Banza.
إرسال تعليق