Binti wa miaka (14) aliyefahamika kwa jina la Latifa amejikuta akisutwa
kwa utapeli baada ya kunaswa na OFM akijifanya ni mtoto asiye na wazazi
wala ndugu wa kumsaidia.Binti huyo aliwasimulia waandishi wetu kuwa
baba yake alimtelekeza kwa majirani huko Dodoma maeneo ya Kibaigwa kwa
kile alichodai kuwa baba yake alikuwa na madeni yaliyosababisha mali
zake kupigwa mnada na yeye kusakwa ndiyo maana alikimbia.
Latifa anayedaiwa kwa utapeli.
Latifa alisimulia kuwa kwa kuwa hakuwa na ndugu yeyote aliyekuwa
akimfahamu alilazimika kuishi maisha magumu ya kuhamahama akiwa peke
yake ambapo alidai alikimbilia kwa ndugu wa baba zake mkoani Lindi
ambapo huko alikutana na kasumba ya ukeketaji na kukimbilia jijini Dar.
Akiwa Dar Latifa aliwasimulia waandishi wetu kuwa alikuwa
akifanyishwa kazi nyingi kama hausigeli ndani ya nyumba moja maeneo ya
Tegeta ambapo pamoja na hayo alikuwa akinyanyaswa sana.
Alizidi kudai kuwa aliamua kukimbilia Kijitonyama akiwa kama
mzururaji ambapo alikutana na madada wanaojiuza ambao alidai kuwa
walimchukua na kuishi naye mpaka alipokutana na waandishi wetu ambao
aliwaomba msaada kwa madai hakuwa na chakula wala mahali pakulala .
Staa katika tasnia ya filamu Bongo, Elizabeth Michael.
AANZA KUSHTUKIWA
Hata hivyo, baada ya kupelekwa kwa mfadhili aliyeahidi kumpa malazi binti huyo, alimshangaza mwenyeji wake kwa kupigiwa simu mara kwa mara na watu ambao hakuwaweka wazi. Alipopekuliwa kwenye simu ndipo namba za watu waliogundulika kuwa ni ndugu zake walionekana na walipopigiwa walikiri kumfahamu Latifa kama ndugu yao na kuanika siri kwa nyakati tofauti kuwa kweli Latifa hana mama lakini tabia za utapeli zimemfanya afukuzwe kwa kila ndugu anayeishi naye.

“Yaani huyo mtoto hakuna mtu anayetaka kuishi naye mimi mwenyewe
ameshaniliza na simtaki aje kwangu, nyie cha msingi mtoeni hapo nyumbani
kwenu yasije yakawakuta,” alisema kaka yake aliyejitambulisha kwa jina
la Saidi kauli iliyotiliwa mkazo na mama yake mdogo aliyejitambulisha
kwa jina la Mwazani.
Jacqueline Wolper.
Hata hivyo, waandishi wetu waligundua kuwa msichana huyo kwa nyakati
tofauti alienda nyumbani kwa wasanii wa filamu, Wema Sepetu, Jacqueline
Wolper na Elizabeth Michael kwa nia ya kutaka wamasaidie lakini
kashitukiwa na kutimuliwa.
“Nilienda kwa Wema nikagonga akatokea msichana akaniambia Wema hayupo
nikawa narudia mara nyingi lakini mwishoni akanifokea. “Nikaenda kwa
Lulu lakini mama yake alinifukuza na kwa Wolper niliambiwa alipokuwa
akiishi alishahama,” alisema msichana huyo aliyedai yote aliyofanya ni
kutokana na ugumu wa maisha hivyo asitiriwe.
Post a Comment