Msanii wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’.
MSANII wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amefunguka kuwa anaamini amepigwa ‘juju’ kutokana na kuugua ugonjwa ambao haukutambulika hospitalini.
Akizungumza
machache na paparazi wetu akiwa nyumbani kwake anapougulia maeneo ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bozi alisema, anaamini amerogwa na
wasanii wenzake wasiopenda maendeleo baada ya kupata dili la kucheza
filamu katika Kundi la Kaole.
“Roho inaniuma sana yaani ni jinsi gani wasanii tulivyokuwa hatupendani, ghafla tu nilipofika nyumbani baada ya kutokea Moro kwenye dili la kazi hali yangu ilibadilika, nikahisi kichwa kuniuma sana na maumivu makali tumboni, nilipoenda hospitali niliambiwa sina tatizo ikanilazimu nitafute mtaalamu na kuyabaini hayo maana lengo lao walitaka kunimaliza, nashukuru Mungu kwa sasa nimepata nafuu,” alisema Bozi.
MSANII wa filamu Bongo, Fatuma Ayubu ‘Bozi’ amefunguka kuwa anaamini amepigwa ‘juju’ kutokana na kuugua ugonjwa ambao haukutambulika hospitalini.
Akizungumza
machache na paparazi wetu akiwa nyumbani kwake anapougulia maeneo ya
Kinondoni jijini Dar es Salaam, Bozi alisema, anaamini amerogwa na
wasanii wenzake wasiopenda maendeleo baada ya kupata dili la kucheza
filamu katika Kundi la Kaole.“Roho inaniuma sana yaani ni jinsi gani wasanii tulivyokuwa hatupendani, ghafla tu nilipofika nyumbani baada ya kutokea Moro kwenye dili la kazi hali yangu ilibadilika, nikahisi kichwa kuniuma sana na maumivu makali tumboni, nilipoenda hospitali niliambiwa sina tatizo ikanilazimu nitafute mtaalamu na kuyabaini hayo maana lengo lao walitaka kunimaliza, nashukuru Mungu kwa sasa nimepata nafuu,” alisema Bozi.

إرسال تعليق