Mwanadada Chiku Ketto a.k.a Chiku K Balaa
ameamua kuweka wazi hisia zake alizonazo kuhusu kile anachokiona
kinamtesa Aliyekuwa Member Mwenzake wa Kundi la LaFamilia.Akizungumza na
Kipindi cha DUNDO cha MamboJambo Radio Arusha kupitia Kipengele cha
DROP BOX Chiku amesema ana mpango wa kukaa Karibu zaidi na Chid Beenz
Kwakuwa anajua anakoelekea sio kwema kwani wakati wakiwa Pamoja Chid
alikuwa na Mafanikio na Hakuwa kama alivyokuwa Kitu ambacho kinaonekana
kama Chid beenz amekosa mtu wakuwa karibu zaidi na yeye kwa Ushauri na
Ukaribu wa Kimawazo Chanya.
Bila shaka mmefuatilia pia Kesi ambayo
ilikuwa inamkabili Chid Beenz ambayo ilikuwa ya Kukutwa na Madawa ya
Kulevya Katika Uwanja wa JK Nyerere Airport na kuachiwa huru kwa Faini
ya sh. 900 000/= za Kitanzania Hivi juzi hii ni moja ya sababu
zinazoonyesha Chid Baanz amefikia kubaya zaidi.UKIWA unakumbukumbu nzuri
sana utakumbuka wakati ule chid akiwa na LaFamilia Team yake hata
kiafya alikuwa Kajaza na hata watu walikuwa wanamuogopa kwa kuwa alikuwa
na Lile Body Flani la Kinako ila kwa sasa hata machalii wanweza
kumchezea Japo Wembamba hauna maana ya kuwa Umeisha na nguvu ila
kiukweli Chid Amepungua sana Kiafya.
Chiku
amemshauri Chid Kuhakikisha Anakumbuka kuna Mama yake, Ndugu zake
Wanamtegemea na pia Jamii nzima inamwangalia na Cha Mwisho akasema
anampenda sana Chid Beenz Kuna ngoma wamefanya kwa Pamoja na
Atahakikisha Kuwa Chid anaepukana na Majanga yanayomwandama.
Katika
Mazungumzo hayo Chiku amepata Pia nafasi ya Kuzungumzia Ngoma zake
Mbili ambazo zinatoka mwisho wa Mwezi huu au mwanzoni mwa mwezi ujao
Ambapo ngoma hizo mojawapo ni PIGA HATUA ambayo ilikuwa itoke mwaka jana
Mwishoni lakini ikashindwa kutoka sababu alizozitaja kuwa ni Matatizo
yaliyokuwa yametokea katika Management yake na Ya Pili ni ngoma ambayo
itakuwa inahamasisha Vijana Kupiga Kura Ukizingatia huu ni mwaka Muafaka
kwa Watanzania Kumchagua Rais Mpya, Wabunge na Madiwani katika Serikali
Kuu ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania.
YOTE ALIYOYAZUNGUMZA CHIKU K YASIKILIZE KWA KU-CLICK LINK HII >>>>> CHIKU K – NAMPENDA SANA CHID BEENZ

Post a Comment