Jezi za wakali wa timu ya Barcelona, Messi na Neymar
Timu za Barcelona na Atletico Bilbao zitaumana katika fainali za kombe
la Copa del Rey tarehe 30 Mei, baada ya kufuzu michezo yao ya nusu
fainali iliyochezwa Jumatano usiku kwa michezo miwili ya nusu fainali.
Barcelona
ilimenyana na Villarreal katika mchezo wa marudiano baada ya ule wa
awali uliopigwa katika dimba la Barcelona la Nou Camp.
Katika
kipute hicho cha jana Barcelona waliwafunga wapinzani wao mabao 3-1 na
kuingia fainali kwa jumla ya mabao 6-2 katika michezo yote miwili
iliyochezwa na timu hizo.
Nayo Atlhletico Bilbao ikaisasambua
Espanyol bao 2-0 na kuweza kuingia fainali kwa jumla ya mabao 3-1 baada
ya kutoka sare ya 1-1 katika mchezo uliopita.
Kwa matokeo hayo sasa Barcelona watavaana na Athletico Bilbao katika mchezo wa fainali utakaopigwa tarehe 30 Mei
إرسال تعليق