Mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Vick Kamata.
Sifa za kitaaluma (CV) za mbunge wa viti maalum kwa tiketi ya Chama cha Mapinduzi (CCM), Vick Kamata zilizopo kwenye tovuti ya Bunge la Jamhuri ya Tanzania, zimezua utata kutokana na ‘makengeza’ zilizonazo.
Habari zilizotua kwenye dawati za Uwazi Mizengwe kutoka kwa chanzo
chetu kabla ya kusambaa kwenye mitandao ya kijamii, zilieleza kuwa sifa
za kitaaluma za mbunge huyo zilizoandikwa kwenye mtandao wa bunge,
zilikuwa na dalili ya kupotosha baadhi ya mambo.
Uwazi Mizengwe liliingia mzigoni na kubaini kuwa CV hiyo ya
Mheshimiwa Vick, ilikuwa ikionesha kwamba mheshimiwa huyo ana shahada ya
pili (masters degree) katika mambo ya utawala na biashara za kimataifa
aliyoipata kwenye Chuo Kikuu cha Southampton Solent cha nchini Uingereza
kuanzia mwaka 2008 hadi 2009.
Pia CV hiyo ilionesha kwamba shahada ya kwanza ya uandishi wa habari
(bachelor degree) aliipata kwenye Chuo Kikuu cha St. Augustine jijini
Mwanza kuanzia mwaka 2001 hadi 2005. Kabla ya hapo, alikuwa na
stashahada (diploma) ya mambo ya kompyuta.
MKANGANYIKO ULIOPO
Katika CV hiyohiyo, kuna maelezo mengine yanayokinzana na ya awali ambayo yanaeleza kwamba mheshimiwa huyo, hana shahada ya uandishi wa habari bali alisomea kozi fupi ya uandishi wa habari (certificate) katika chuo hicho kilichopo jijini Mwanza kuanzia mwaka 2000 hadi 2001.
Katika CV hiyohiyo, kuna maelezo mengine yanayokinzana na ya awali ambayo yanaeleza kwamba mheshimiwa huyo, hana shahada ya uandishi wa habari bali alisomea kozi fupi ya uandishi wa habari (certificate) katika chuo hicho kilichopo jijini Mwanza kuanzia mwaka 2000 hadi 2001.
Mkanganyiko mwingine uliopo, ni kwamba kama ni kweli mheshimiwa huyo
hakuwa na shahada ya kwanza ya uandishi wa habari, isingewezekana kwenda
kuchukua shahada ya pili nchini Uingereza kwani kisheria, ni lazima uwe
na shahada ya kwanza ndiyo ukasomee ya pili.
“Haiwezekani mtu mwenye diploma (shahada) tena ya kawaida tu aende
kuchukua masters, ni lazima awe kwanza na digrii au advanced diploma,”
alichangia mdau mmoja wakati akichangia mada hiyo mtandaoni.
Baada ya kujiridhisha juu ya mkanganyiko huo, Uwazi Mizengwe
lilimtafuta mbunge huyo ili atoe ufafanuzi lakini simu yake ya mkononi
haikuwa ikipatikana hewani. Juhudi za kumtafuta bado zinaendelea na
atakapopatikana, atatoa ufafanuzi kuhusu mkanganyiko huo.

إرسال تعليق