EXCLUSIVE: Zitto ajiunga rasmi na Chama cha ACT-Tanzania, akabidhiwa kadi namba 007194

Mh. Zitto Kabwe akilipa kwa ajili ya usajili wa kadi ya uanachama wa ACT.
...Kumwaga ‘mboga’ mbele ya wandishi wa Habari Jumapili hii Machi 22
Na Andrew Chale wa Modewji blog
Hayawi hayawi…Sasa yamekuwa licha ya kusemwa sana kwa muda mrefu juu ya kuhusishwa na chama kipya cha siasa cha ACT-Tanzania dhidi ya aliyekuwa Mbunge wa Kigoma Kaskazini Zitto Ruyagwa Kabwe sasa yamekuwa kweli kwa Mbunge huyo baada ya leo Jumamosi ya Machi 21, kupokelewa rasmi na chama hicho na kukabidhiwa kadi yake yenye namba 007194.
Hii  inafuatia siku moja baada ya Zitto kutangaza kuachia ubunge na kuandika barua rasmi ambapo sasa amekuwa mwanachama wa ACT-Tanzania na kuahidi kuendeleza mapambano ndani ya chama hicho.
_MG_7798
Mh. Zitto Kabwe akisaini kadi ya uanachama wa ACT.
Hata hivyo, kwa mujibu wa viongozi waandamizi wa ACT-Tanzania wamedokeza kuwa, Zitto ataongea na vyombo vya habari Jumapili ya Machi 22.
Endelea kufuatilia Hisia za Mwananchi kwa tukio hilo tutakalowaletea kila kitakachojiri katika mkutano huo, kujua ni wapi na muda gani  endelea kuperuzi nasi.
ACT-Tanzania: kirefu chake ni :  Chama cha Alliance for Change and Transparence (ACT-Tanzania). Makao makuu ya chama hicho yapo Kijitonyama Jijini Dar es Salaam, Tanzania.
_MG_7819
Mh. Zitto Kabwe akikabidhiwa rasmi kadi ya uanachama wa ACT.
_MG_7825
Mwanachama rasmi wa ACT Mh. Zitto Kabwe akipokea kadi hiyo.
_MG_7829
“He..he he mnipokeee sasa kwa mikono miwili….:, Mh. Zitto Kabwe akionyesha kadi hiyo kwa baadhi ya wanachama waliosimama (hawapo pichani) nje ya ofisi za chama cha ACT tawi la Tegeta,
_MG_7858
Mh. Zitto Kabwe akibadilishana mawazo na viongozi wa Chama cha ACT mara baada ya kupokea kadi hiyo.
_MG_7864
Mh. Zitto Kabwe akiwa amefuatana na Prof. Kitila Mkumbo ambaye pia ni mwanachama wa ACT.
_MG_7893
Mh. Zitto Kabwe akivalishwa skafu ya ACT mara baada ya kupokea rasmi kadi ya chama hicho mapema JANA.
_MG_7958
Na hii ndio kadi rasmi ya Mheshimiwa Zitto Kabwe aliyokabidhiwa.

Post a Comment

Previous Post Next Post