Umoja
wa Vyama vya wanafunzi elimu ya juu kutoka vyuo mbalimbali kanda ya
kaskazini Kilimanjaro na Arusha wajitokeza kumshawishi Prof. Sospeter
Muhongo kugombea urais wa Jamhuri ya muungano wa Tanzania Mwaka
2015.(Picha na Jamiiblog).
Akizungumza
kwa niaba ya vijana wenzake Mwenyekiti wa vijana Charles Ngereza
kutoka chuo cha Uhasibu Arusha amesema kuwa kinachowafanya kumshawishi
Prof Sospeter Muhongo kugombea urais ni kutokana na kuwa kiongozi bora
kwa wananchi na mtu anayejali matatizo ya wananchi katika kuwapatia
huduma.
Pia
wanasema kuwa amekuwa akiwezesha uchumi kujitegemea na kupinga
ulanguzi katika sekta ya uwekezaji pamoja na kutetea vijana katika
uwekezaji na kupata ajira.
Vijana
hao ambao ni umoja wa vyama vya wanafunzi wa elimu ya juu katika picha
kutoka kushoto ni Nelson Wilson Machumu ,Tumaini University. 2 Daud
Hipolity Shayo Chuo cha Uhasibu (Iaa)3 Sarah Aminirabi Mushi Arusha
University 4. Charles Ngereza Chuo Cha Uhasibu Arusha.5. Hobeshi
Juvenary Makumira University Pamoja na Rahma Yusuph Sengeza Chuo cha
Jomo Kenyata.
Post a Comment