FAMILIA
ya mzee Wilson Lyimo, mkazi wa maeneo ya Sinza-Makaburini, jijini Dar,
imejikuta ikilala nje kwa wiki kadhaa baada ya kuvunjiwa nyumba yao
usiku wa manane na watu wanaodaiwa kuwa ni mabaunsa wapatao 60.
Vitu vikiwa nje baada ya nyumba kuvunjwa.
Mabaunsa hao wanadaiwa kufanya tukio hilo usiku wa kuamkia Februari
24, mwaka huu wakati wanafamilia hao pamoja na wapangaji wawili wakiwa
wamelala ndani ya nyumba hiyo.
Chanzo makini kimeeleza kuwa, mabaunsa hao walipofika kwenye nyumba hiyo, waliamuru watu wote waliokuwa ndani watoke nje wakidai wamepewa maagizo ya kuvunja nyumba hiyo na jamaa mmoja (jina tunalihifadhi kwa sasa).

Mabaunsa hao walianza kubomoa kuta za nyumba hiyo bila kujali watoto
na wapangaji kama wametoka nje au la ambapo hali hiyo ilisababisha
usumbufu na upotevu wa baadhi ya vitu ambavyo thamani yake haikupatikana
mara moja.

Kundi
hilo la watu waliokuwa na nyundo na sururu waliendelea kuvunja nyumba
hiyo huku wakitembeza kipigo kwa yeyote aliyejitokeza kutaka kuzima
zoezi lao la kubomoa.
Kwa mujibu wa mtoto wa kwanza wa familia hiyo, Edwin Lyimo, baba yake
anamiliki eneo hilo kihalali tangu mwaka 1977 kwa namba ya kiwanja
Block C Namba 68, Namba ya Hati 21818 yenye jina la usajili, Wilson
Fataeli Lyimo.
Edwin aliendelea kufunguka kuwa, awali familia hiyo ilikuwa na
mgogoro wa muda mrefu na jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao kuhusu kiwanja
na nyumba hiyo hadi kufikishana Mahakama ya Ardhi lakini ghafla
wameshangaa kuona mabaunsa hao wamekuja kuvunja nyumba hiyo.
Akizungumza
na waandishi wetu, mzee Lyimo alidai kuwa nyumba hiyo ni yake na hati
anazo na kuongeza kuwa anashangazwa na watu hao waliovamia na kuvunja
nyumba yake na kuahidi kuwachukulia hatua ambapo amefungua jalada kituo
cha polisi Mabatini lililosomeka KJN/2050/2015/KUVUNJA NA KUIBA USIKU.
Waandishi wetu walifika eneo la tukio na kukuta nyumba ya familia
hiyo ikiwa imebomolewa huku wenyewe wakiweka mahema ili kujisitiri na
mvua na jua huku wakiwa hawana msaada wowote.
Jitihada za kumpata jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao ili aweze kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana hewani, jitihada zinaendelea.
Jitihada za kumpata jamaa aliyetajwa na mabaunsa hao ili aweze kuzungumzia sakata hilo hazikuzaa matunda kutokana na simu yake kutopatikana hewani, jitihada zinaendelea.

إرسال تعليق