Mwanamume
mmoja amekutwa na kuondolewa funza wapatao mia moja walio hai tena
wanao kula kula puani mwake na kuruhusiwa aende nyumbani .Mwanamume huyo
anatajwa kuwa na umri wa miaka sitini na mitano ,na watabibu wanasema
funza hao walikuwa wamejichimbia ndani zaidi ya pua yake.
Mwanamume
huyo ni mwenye asili ya Sao Paulo, nchini Brazil,alikuwa akisumbuliwa
mno na njia ya mfumo wa hewa hasa puani ,na pua yake ilikuwa imeathiriwa
na mabuu ya inzi.
Pamoja na mambo mengine, mara kwa mara mwanaume
huyo alikuwa akilalamika kuwa kuna minyoo pia huwa inadondoka kutoka
puani mwake.
Tundu za pua ni mahali ambapo vijidudu virukavyo huweza kutaga mayai yao hapo na baadaye hugeuka kuwa funza.
Na
wataalamu wa pua na koo wanasema kwamba chakula kikuu cha funza wakaao
puani ni nyama za pua na endapo mgonjwa ataachwa bila kupatiwa matibabu
,funza hao wanauwezo wa kutafuna na kuharibu kabisa mfupa wa mwanzi wa
pua,kuharibu vimishipa vya uso,pua na macho.
Na hali hiyo
ikitokea,jua kutakuwa na maambukizi kwenye ubongo na macho na kwa
kawaida husababisha ugonjwa wa uti wa mgongo na hata kifo.
Mwanaume
huyo aliamua kwenda kwenye zahanati nchini Brazil kutoa malalamiko yake
kwamba siku mbili nyuma aliona kitu kinachofanana na mnyoo ukichomoza
na hatimaye kutoka katika pua yake upande wa kushoto.
Mwanaume huyo anaishi na virusi
vya ukimwi ana tatizo la ini,na kinga yake ya mwili ilikuwa inapungua
kwa kasi kubwa na alikuwa hajaanza kutumia vidonge vya kurefusha maisha.
Miaka
mitano iliyopita alifanyiwa upasuaji wa pua yake baada ya kugundulika
kuwa alikuwa na uvimbe puani na hakuona dalili yoyote hapo kabla,ingawa
kwa wiki nzima kabla ya kuhudhuria zahanati alikuwa akitokwa na damu
puani,maumivu ya pua upande wa kushoto
Na harufu mbaya,alikuwa akishindwa kupumua sawa sawa na uvimbe ulianza kuonekana usoni na puani mwake.
Lakini baada ya kudumbukiza kijikamera kidogo puani mwake ,aligundulika
Madaktari wakaanza kuwatoa funza hao kwa muongozo wa kamera iliyokuwa ikiangaza puani na kuitibu pua yake.
Iliwachukua
siku nne madaktari kuondoa uambukizo katika pua ya mwanaume huyo na
baada ya hapo madhila yake yakakoma na baada ya uangalizi wa mwisho kwa
kutumia kamera ile ile imethibitika kwamba tatizo lake lime kwisha

إرسال تعليق