![]() |
Miili ya watu 7 wa familia moja waliokufa katika tukio hilo |
Watu
35 walifariki dunia papo hapo na wengine wakiwa hospitali ya wilaya ya
Kahama kutokana na mvua kubwa iliyoambatana na upepo na mawe
yanayodaiwa kuwa na ukubwa mithili ya ndoo ndogo ya lita kumi katika
kijiji na Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga usiku wa
kuamkia le mvua hiyo imenyesha kwa muda wa takribani dakika 30,imeua pia mifugo wakiwemo ng’ombe na mbuzi na kuharibu vibaya mimea.
Afisa
mtendaji wa kata ya Mwakata Mahega Mwelemi ameiambia Malunde1 blog kuwa
maeneo yaliyoathirika kuwa ni cha Mwakata,Nhumbi na Magung’humwa.
Mwelemi amesema watu wengi wamefariki kwa kuangukiwa na nyumba zao,kuzidiwa na maji pamoja kupigwa mawe ya mvua ambayo hadi leo asubuhi yalikuwa yanaonekana kijijini hapo.
Mwelemi amesema watu wengi wamefariki kwa kuangukiwa na nyumba zao,kuzidiwa na maji pamoja kupigwa mawe ya mvua ambayo hadi leo asubuhi yalikuwa yanaonekana kijijini hapo.
Mkuu
wa wilaya ya Kahama Benson Mpesya aliyefika eneo la tukio bado
wanafanya ukaguzi katika kila kaya kubaini idadi ya watu waliofariki
dunia,kujeruhiwa na idadi ya mifugo iliyokufa.
![]() |
Awali Kamanda wa polisi mkoa wa Shinyanga Justus Kamugisha amesema kuwa idadi ya vifo na majeruhi inaweza kuongezeka.
Hata hivyo Mkuu wa mkoa wa Shinyanga Ally Rufunga aliyefika eneo la tukio amesema waliofariki dunia ni hadi sasa ni 41 ,majeruhi 91 na jumla ya watu waliothirika na tukio hilo ni 4,291 kuongeza kuwa kinachohitajika sasa ni misaada mbalimbali ya kibinadamu.

Amesema
Mvua hiyo ambayo ilinyesha kwa muda mfupi imewaacha watu 3,500 bila
makazi katika kaya 350 huku nyumba zikifurika maji na baadhi ya mifugo
ikisombwa.
Amesema
mali mbalimbali zimeharibiwa vibaya ikiwemo mifugo kuzolewa na maji na
vyakula kwenye eneo lote lililokumbwa na mafuriko hayo.
Hali ya majeruhi ambao wamepelekwa katika hospitali mbalimbali bado sio nzuri kwa baadhi ingawa wengine wanaendelea vizuri.
Kamanda
wa jeshi la zimamoto na uokoaji mkoa wa Shinyanga Elisa Mugisha amesema
baada ya kupata taarifa kuwepo kwa tukio hilo walifika katika eneo la
tukio kwa ajili ya uokoajI
Rais
Jakaya Kikwete amemtumia salamu za rambirambi mkuu wa mkoa wa
Shinyanga, Bw. Ali Nasoro Rufunga kuomboleza vifo vya watu 42 huku
wengine 91 wakijeruhiwa usiku wa kuamkia tarehe 4 Machi, 2015.
Tukio hilo la kusikitisha limetokea katika kata ya Mwakata iliyoko katika wilaya ya Kahama mkoani Shinyanga kufuatia mvua kubwa ya mawe iliyonyesha ikiambatana na upepo mkali na kuathiri watu 3,500.
Katika
kata Mwakata iliyoathiriwa zaidi, kaya 350 zimeathiriwa katika kijiji
cha Makata wakati katika kijiji cha Nhumbi, kaya 100 zimeathirika.
Katika kijiji cha Magung'hwa, kaya 50 zimeathiriwa.
Rais Kikwete amesema msiba huo siyo wa wana-Shinyanga pekee bali ni wa taifa zima ambalo limepoteza nguvu kazi muhimu kwa maendeleo yake na ustawi wa jamii ya watanzania kwa ujumla.
Rais
Kikwete amewaomba wafiwa wote wawe na moyo wa uvumilivu, utulivu na
subira wakati huu wa majonzi makubwa kwao wanapoomboleza vifo vya ndugu
na jamaa zao.
Rais Kikwete amesema msiba huo siyo wa wana-Shinyanga pekee bali ni wa taifa zima ambalo limepoteza nguvu kazi muhimu kwa maendeleo yake na ustawi wa jamii ya watanzania kwa ujumla.
![]() |
Mwananchi akiwa amebeba moja ya barafu la mvua,yaliyokuwa yanadondoshwa na mvua kubwa iliyonyesha usiku wa kuamkia leo katika Kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga. |
Aidha
amewahakikishia wafiwa wote kuwa binafsi yuko pamoja nao katika kipindi
chote cha kuomboleza msiba huu mkubwa kwao na kwa taifa

Kufuatia
tukio la kusikitisha na kuhuzunisha lililotokea usiku wa kuamkia Machi
4,2015 huko katika kata ya Mwakata wilayani Kahama mkoani Shinyanga la
watu 42 kupoteza maisha na wengine 91 kujeruhiwa kutokana na mvua kubwa
iliyokuwa imeambatana na upepo na mawe,mbunge wa Jimbo la Msalala
kulikotokea tukio hilo,Mheshimiwa Ezekiel Maige,amezungumzia tukio hilo.
Alichokisema hiki hapa chini:
Nimepokea
kwa mshituko mkubwa taarifa za mvua kubwa, yenye upepo na theluji
nyingi iliyonyesha kwa muda wa dakika 35 tu saa 5 usiku wa kuamkia leo
Jumatano Machi 4,2015.
Nimepata taarifa za tukio hilo nikiwa safarini Kigoma kikazi na Kamati ya Hesabu za Serikali za Mitaa ambayo mimi ni mjumbe.
Kutokana
na uzito wa tukio hili nimesitisha ziara hiyo na kuondoka Kigoma majira
saa 5 asubuhi na hivyo kufika Mwakata saa 2 usiku huu.
Hali niliyoikuta kama wengi walivyokwishatoa ushuhuda ni ya kusikitisha na kushangaza sana.
Sijawahi kuona maafa yatokanayo na mvua katika jimbo langu miaka yote niliyoishi hapa.
Maafa ni makubwa yasiyoelezeka.
Naomba kusema yafuatayo:-
Kwanza, nawapa pole sana familia zote zilizopoteza wapendwa wetu.
Mungu awarehemu wapendwa ndugu zetu waliopoteza maisha katika tukio hili.
Aidha namuomba Mungu atupe moyo wa ujasiri kuikabili hali hii na atupe nguvu za kusimama haraka na kurejea kwenye hali ya maisha yetu ya kawaida.
Pia namuomba Mungu atuepushe na mitihani ya kiwango hiki ambayo kwa kweli ni mizito.

Pili, nawashukuru
sana viongozi wa serikali na Chama, wakiongozwa na Mwenyekiti wa Kamati
ya maafa wilaya ya Kahama ambaye ni mkuu wa wilaya ya Kahama Benson
Mpesya kwa juhudi kubwa walizofanya kuokoa majeruhi na kusaidia wahanga.
Wamefanya kazi kubwa sana kwani, hadi jioni nilipofika kwenye eneo la tukio, majeruhi wote 91 walikuwa wamefikishwa hospitalini na walikuwa wanaendelea kupata matibabu na miili ya marehemu kadhaa ilikuwa imeanza kuzikwa.
Aidha nawashukuru kwa kusaidia vitu mbalimbali ikiwemo vyakula.

Tatu, nawashukuru
sana watu wote wenye mapenzi mema ambao wameanza kutupatia misaada
mbalimbali ikiwemo unga, mablanketi, sukari, mikate na vinywaji
mbalimbali.
Nawaomba watu wote wenye mapenzi mema waendelee kusaidia kwani waathirika ni wengi, zaidi ya 4,000 hivyo hali itazidi kuwa mbaya jinsi siku zitakavyosonga mbele endapo ndugu zetu hawatapatiwa msaada.
Nawaomba watu wote wenye mapenzi mema waendelee kusaidia kwani waathirika ni wengi, zaidi ya 4,000 hivyo hali itazidi kuwa mbaya jinsi siku zitakavyosonga mbele endapo ndugu zetu hawatapatiwa msaada.
Nne, mimi
kama Mbunge wa eneo husika, pamoja na kusikitishwa na tukio hili, natoa
wito kwa serikali, hasa Ofisi ya Waziri Mkuu kitengo cha maafa,
makampuni, taasisi, mashirika na watu binafsi wasaidie kwa haraka
misaada ya chakula, mavazi na makazi kwa waathirika.
Binafsi nitawasilisha msaada wangu wa tani 5 za unga kesho asubuhi tarehe 5,Machi ,2015 .
Binafsi nitawasilisha msaada wangu wa tani 5 za unga kesho asubuhi tarehe 5,Machi ,2015 .
Tano, naomba
sana watu wote wenye mapenzi mema wasaidie kurudisha maisha ya
waathirika kwenye hali ya kawaida hasa kwa kuwasaidia vifaa vya ujenzi
kama mbao, bati na theluji.
Sita, ombi
maalum kwa serikali, naomba sana serikali itoe punguzo maalum la ushuru
kwenye simenti, nondo na mabati kwa wananchi wote wa Kahama ambao wengi
wao wana nyumba za tope zilizoezekwa kwa nyasi, na hivyo kutokuwa imara
kuhimili upepo mkali au mvua kubwa.
Inavyoonekana, mabadiliko ya tabia nchi sasa ni dhahiri kwamba matukio ya kimbunga au mvua kubwa zenye upepo yanazidi kuongezeka Kahama, kwani ni wiki moja tu imepita tangu mvua yenye upepo iliponyesha kwenye kijiji changu cha Segese ambapo nyumba zaidi ya 50 zilianguka au kubomoka na nyingine nyingi kuezuliwa mapaa.
Tukio hilo liliathiri hata nyumbani kwa mzazi wangu ambapo ukuta wa uzio ulianguka!

Ukiangalia maeneo yaliyoathirika, idadi kubwa ya nyumba zilizoanguka ni nyumba za tope zilizoezekwa kwa nyasi.
Hivyo maafa yanakuwa makubwa maeneo yetu haya kutokana na nyumba zetu kutokuwa imara.
Hivyo ni lazima sasa wananchi wetu tuwasaidie kujenga nyumba imara zinazohimili upepo mkali na mvua zenye dhuruba hali inayoonekana kuwa ikijirudiarudia.

Kwa mara nyingine natoa pole sana kwa wote na kuwaomba wadau wote wasaidie kwa kadiri watavyoweza.
Misaada yote ipelekwe kwa Mkurugenzi wa Halmashauri ya Wilaya ya Msalala au Mkuu wa Wilaya ya Kahama.
![]() |
Post a Comment