Hiki Ndicho Alichokisema Mkandarasi na Mkubwa Fella kuhusu kuanguka ukuta wa nyumba ya Diamond #U Heard



Kutokana na mvua kubwa zinazoendelea kunyesha nchini na kuleta madhara mbalimbali kuna taarifa kuwa nyumba ya kifahari ya msanii Diamond Platnumz ambayo  ujenzi wake haujakamilika imekubwa na madhara ya mvua baada ya ukuta wake kuanguka.

Mtaalam wa majengo fundi Saidi amesema, tukio kama hilo linaweza kutokea kutokana kuto kumwagwa zege chini na juu hunaweza kukawa hapakufungwa mkanda lakini mpaka aione ndio anaweza kujua chanzo cha tatizo.

Soudy Brown alimtafuta Diamond bila mafanikio na kuamua kumtafuta meneja wake Said Fella, ambae amesema kuwa hataweza kuzungumzia kwasababu nyumba hiyo kakabidhiwa mkandarasi, ila ni kweli ukuta umeanguka kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha lakini bado iko chini ya mkandarasi na anatakiwa kukabidhi mwezi wa sita, ingawa Diamond ameshahamia kwenye nyumba hiyo mwezi mmoja uliopita lakini hakupata madhara yoyote kutokana na tukio hilo.

Ili kusikiliza story yote bonyeza play hapa chini…

Post a Comment

Previous Post Next Post