Mahakama ya juu nchini India imefutilia mbali uwezo wa polisi kuwashtaki watu kutokana na maoni yao ya Facebook.
Mahakama
ya juu nchini India imefutilia mbali kipengee cha sheria kali iliyowapa
polisi uwezo wa kuwashtaki watu kutokana na maoni yao kwenye mtandao wa
kijamii wa Facebook.
Mahakama ya juu zaidi nchini humo imesema
kuwa kipengee hicho cha 66A iliyolenga kudhibiti sekta ya utandawazi
ilikuika katiba ya taifa na haswa kipengee cha uhuru wa kujieleza.
Katika
miaka ya hivi karibuni ,watu wengi wamejipata matatani kutokana na semi
zao na maoni kwenye mitandao ya kijamii ya Facebook na Twitter.
Serikali
ilikuwa inajitetea kwa kusema kuwa sheria hiyo kali ilikuwa ikilenga
kudhibiti visa vya raia kuweka habari za chuki na matusi kwenye mitandao
ya kijamii.
Uamuzi huu wa mapema leo ulitolewa na majaji wawili
kufuatia ombi la rufaa kutoka kwa wanaharakati wa haki za kibinadamu
nchini humo
na mwanafunzi wa sheria katika chuo kikuu kimoja
nchini humo ambao walilalamika kuwa sheria hiyo ilikuika uhuru wa
kujieleza uliokuwa umelindwa na katiba ya nchi.
"kipenge cha 66A kinakiuka katiba na hivyo ninaamuru kifutiliwe mbali ''shirika la habari la AFP lilimnukuu jaji RF Nariman.
"haki ya kikatiba ya raia wote kufahamishwa inakiukwa kwa sehemu kubwa tu'' aliongezea.
Mahakama kuu ya India

Kulingana na kipengee hicho,66A wahindi walioikashifu serikali idara zake wangelishikwa na kufungwa hata kwa miaka mitatu.
Wanaharakati wanasema kuwa mtu angeweza kufungwa kwa ''kutuma barua ambayo ingezua mjadala mkali na kusababisha usumbufu''
Sheria
hiyo ilipingwa vikali na mwanafunzi huyo mwaka wa 2012 baada ya
wasichana wawili kukamatwa Mumbai kwa kutoa maoni yao kufuatia mauaji ya
mwanasiasa maarufu Bal Thackeray.
Shaheen Dhada alikamatwa kwa kukashifu hatua ya serikali kuimarisha usalama mjini Mumbai punde baada ya kifo chake Thackeray.
Kwa upande wake Renu Srinivasan, alikamatwa kwa ku'like''ujumbe huo.
Kumekuwa na idadi kubwa ya wanaharakati waliokamatwa kwa kutumia sheriahiyo inayodaiwa kuwa katili.
Post a Comment