Hofu ya uvamizi wa kundi la Panya Road kwa mara nyingine
iliwakumba wakazi wa Tabata Machi 10 na kusababisha shughuli mbalimbali
kusimama.
Katika kupata undani wa asili ya makundi hayo ya
uhalifu, mwandishi wetu amezungumza na kijana aliye katika kundi la
Panya Road la Tabata, Mtaa wa Twiga, (jina linahifadhiwa) ambaye
anaeleza jinsi vikundi hivyo vinavyoundwa hadi kufanya uhalifu.
Vigodoro/mnanda/kamari
Anasema kwanza vijana huanzisha kundi la watu
wachache, ambalo huanza kwa kucheza katika sherehe mbalimbali usiku,
wakati mwingine whutunga nyimbo kwa madai ya kutaka kurekodi.
Baada ya vijana hao kuwa kundi kubwa huanza kupanga njama za uhalifu.
“Kwenye makundi haya, kuna wengine hawajawahi
kuvuta bangi, wanajifunzia hapo, wengine hawajawahi kunywa pombe,
wanajifunza hapo. Hapa ndipo tunaanza kuambiana namna ya kukaba na aina
zote za kabali utazijua,” anasema.
napotokea kuna eneo lina sherehe au ngoma ya
kigodoro, hapo ndipo kundi hupata kazi ya kufanya kwa sababu uhalifu
hufanyika nyakati za usiku.
“Kwenye vikundi vyetu tunakuwa na umoja wenye
nguvu, hatuwezi kukubali mmoja wetu akapata tatizo tukamwacha. Mwenzetu
akifanyiwa kitu lazima tulipize kisasi,”anasema
Anatoa mfano tukio la uhalifu wa Machi 10 na kuuwa
kwa kijana Amiri Hega (16) na kusema: “Hega sawa ameiba, lakini
‘postmorterm’ (uchunguzi wa madaktari) inaonyesha alitobolewa macho. Kwa
nini wafanye hivyo?” anahoji kijana huyo mwenye umri wa miaka 22.
Mkazi wa Tabata, Kimanga, Ally Aesha au Chollo
anasema makundi hayo yamesababisha ukosefu wa amani katika maeneo ya
Vingunguti, Tabata, Buguruni na Segerea.
“Hapo Twiga, usijaribu kupita kuanzia saa tatu usiku. Ni hatari. Ni vijana wadogo, lakini wanaweza kukuua,” anasema Chollo.
Kauli ya RPC Wambura
Post a Comment