Mvua ya DAR, walichosema TANESCo.. #Urais2015.. Magari ya Utalii kuingia Kenya? #PowerBreakfast (sauti)

Kwenye zile zilizoandikwa magazetini na kuchambuliwa kwenye Power Breakfast @CloudsFM leo March 23, iko story ya watu watano kufariki kutokana na mvua iliyonyesha Dar, makundi mbalimbali kuibuka uchaguzi wa Urais 2015 na stori ya albino kulindwa kwa teknolojia ya simu ya mkononi.
BAKWATA yakana kauli iliyotolewa hivi karibuni na Sheikh wa Mkoa wa Dar, Alhadi Mussa Salum, Sakata la magari ya Tanzania yanayobeba watalii nchini Kenya lafikiwa muafaka, ukosefu wa damu katika Hospitali mbalimbali nchini unaweza kusababisha madhara makubwa, kesi inayowakabili vigogo wa MSD inatarajiwa kusikilizwa leo na wanawake wa Tanzania na Nigeria vinara wa kutumia mkorogo.
Kulikuwa na interview na Waziri wa Mambo ya Nje na Ushirikiano wa Kimataifa, Bernard Membe ambaye amezungumzia mazungumzo yalifoyanyika kati ya Serikali ya Tanzania na Kenya kuhusu sekta ya utalii na sekta ya uchukuzi na kufikia maamuzi wa magari yote ya utalii Tanzania kuruhusiwa kuingia Kenya kuchukua watalii kama ilivyokuwa awali na usafiri wa ndege za Kenya kundelea na safari zake 42.
Mkurugenzi Mtendaji wa TANESCo Mhandisi Felchesmi Mramba amesema mvua kubwa iliyonyesha imeleta madhara makubwa ikiwemo kusababisha vifo na kutoa tahadhari kwa wananchi kutokana na mvua zinazoendelea kunyesha nchini wasiguse wala kusogelea waya wowote uliodondoka.
Kusikia stori hizi zote na nyingine bonyeza play hapa

Post a Comment

Previous Post Next Post