MTOTO aitwaye Badru Muhidin mwenye umri wa miaka miwili, amepata pigo kubwa baada ya kukatwa uume wake kimakosa na babu yake aliyekuwa amempeleka kutahiriwa kienyeji huko Mbagala jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki iliyopita.
Mtoto aitwaye Badru Muhidin akiwa na mama yake.
Mama mzazi wa mtoto huyo, Mwajuma Hussein ambaye ni mkazi wa Yombo
jijini Dar, alisema aliishi na mwanaye peke yake bila baba yake kwani
walitengana Juni mwaka jana baada ya kuishi bila kufunga ndoa kwa muda
mrefu, lakini mara kwa mara alikuwa akimpeleka mwanaye nyumbani kwa
wazazi wa mumewe kuwasalimia.
“Wiki iliyopita babu yake Eliyasa alimuomba ili wakakae naye kwa muda
mfupi, baada ya muda mfupi walimtuma mtu akaniambia kuwa
wameshamtahiri, nilishangaa sana kwa kuwa hawakunitaarifu juu ya uamuzi
huo, nikaenda kumuona lakini wakawa wananikataza kumtazama sehemu za
siri wakidai mila zao haziruhusu kwa kipindi cha mwezi mzima.
Mtuhimiwa (mwenye fulana nyeupe) akiingia kituoni.
“Kutokana na shauku ya kutaka kuthibitisha hilo, siku hiyo nilipofika
tu nilimchukua na kumtazama hilo eneo ndipo nikabaini kuwa alikuwa
amekatwa katika kichwa, huenda huyo ngariba hakuwa mzoefu, kamfanyia
kienyeji lakini wengine wakisema huenda walitaka kufanya mambo ya
kishirikina,” alisema mama huyo.
Alisema baada ya kumkuta katika hali hiyo, alianza kuhangaika naye
hospitalini kutafuta msaada, alipofika Temeke aliambiwa na
madaktari.kwamba kijana wake alikatwa vibaya na hivyo analazimika
kufanyiwa upasuaji ili kumnusuru.
Babu wa mtoto huyo anashikiliwa na Jeshi la Polisi baada ya
kufunguliwa shauri katika Kituo cha Polisi Mbagala Kizuiani kwa madai ya
ukatili kwa faili namba UKATILI WA MTOTO/MBL/RB/2251/2015 4/3/2015.

إرسال تعليق