Rais Barrack Obama wa Marekani na waziri mkuu wa Israel Benjamin Netanyahu
Rais Obama amepuuzilia mbali onyo alilotoa waziri mkuu wa Israel kuhusu
mpango wa Iran wa Nuclear katika hotuba yake tata kwa bunge la
Marekani.
Bwana Obama amesema Benjamin Netanyahu alishindwa kutoa
suluhisho mbadala kuhusu suala kuu la jinsi ya kuizuia Teheran kutengeza
silaha za Nuclear.
Bwana Netanyahu ambaye alialikwa kuhutubia
bunge na viongozi wa chama cha Republican alishutumu mkataba uliowekwa
kati ya mataifa ya magharibi na Iran na kudai kuwa ni hatari .
Iran imesema kuwa hotuba hiyo ilikuwa ikiudhi na ni ya kujirudia.
Waziri
wa mambo ya nje wa Marekani , John Kerry, anatakiwa kusafiri Saudi
Arabia leo Jumatano kuhakikishia mataifa ya ghuba kuwa mkataba huo
utaimarisha nafasi ya Iran katika eneo hilo.

إرسال تعليق