Kundi la Islamic State
linasema kuwa wapiganaji wake waliendesha mashambulizi ya kujitoa
mhanga kwenye misikiti miwili nchini Yemen ambapo zaidi ya watu 130
waliuawa.
Washambuliaji wanne wa kujitoa mhanga walilenga waumini kwenye mji mkuu Sanaa wakati wa maombi ya Ijumaa.
Maeneo hayo mawili hutumiwa na waumini wanaowaunga mkono waasi wa
Shia wanaofahamika kama Houthi ambao walichukua udhibiti wa mji wa Sanaa
mwaka uliopita.
Zaidi ya watu 200 walijeruhiwa wakati wa mashabulizi hayo ambapo wito wa kuwaomba watu kutoa damu umekuwa ukitolewa.
CHANZO: BBC SWAHILI
Post a Comment