Jeshi la Marekani linasema kuwa linawajulisha karibia wanajeshi 100
waliotajwa kwenye orodha ya mtandao ulioanzishwa na Islamic State
unaotaka wauawe.
Kitengo cha kudukua mitandao cha Islamic State
kinawataka wale wanaolipendelea kundi hilo kuwaua wale walio kwenye
orodha hiyo ambao Islamic State inawalaumu kwa kuendesha mashambulizi ya
angani dhidi yake nchini Iraq na Syria.
Majina yao, picha na namba zao zimechapishwa kwenye mitandao.
Kitengo cha ujasusi cha jeshi la wanamaji la Marekani kinasema kuwa tishio hilo halijathibishwa rasmi .
Kitengo hicho kinawataka wanajeshi kuchukua tahadhari kuhusu ujumbe unaowahusu wanaoweka kwenye mitandao(BBC)
Post a Comment