Na. Johary Kachwamba – MAELEZO, DODOMA
JAMII
imetakiwa kutoa ushirikiano kwa jeshi la polisi nchini katika kutoa
taarifa zitakazo fanikisha kukamatwa kwa wote walioshiriki mauaji ya
watu wenye ulemavu wa ngozi nchini.
Wito
huo umetolewa na Naibu Waziri wa Mambo ya Ndani Mhe. Pereira Silima
(pichani) bungeni mjini Dodoma alipokuwa akijibu swali la nyongeza la
Mhe. Al -Shaimaa Kwegyir, Mbunge wa Viti Maalum aliyehoji kuchelewa kwa
taarifa ya kupatikana kwa mtoto mwenye ulemavu wa ngozi, Pendo Emmanuel.
“Pendo
alitekwa kutoka mikononi mwa mama yake mzazi, hii changamoto ni kubwa
sana, tunaomba jamii itusaidie kutoa taarifa zitakazo saidia kufanikisha
kukamatwa kwa wahusika, tushirikiane kwa pamoja kukomesha tatizo hili”
alisema Mhe. Silima
“tangu
kutekwa kwa mtoto Pendo watu 14 wanashikiliwa na jeshi la polisi
akiwemo baba mzazi, uchunguzi bado unaendelea na watuhumiwa watafikishwa
mahakamani hivi karibuni, ila Pendo bado hajapatikana” aliongezea Mhe.
Silima
Aidha
akijibu Swali la msingi la Mhe. Salumu Barwany, Mbunge wa Lindi Mjini,
aliyehoji idadi ya kesi za mauaji ya walemavu wa ngozi na sababu za
kuchelewa kutolewa hukumu. Mhe. Silima alisema kesi 10 zinaendelea
kisikilizwa mahakama mbalimbali
“kati
ya mwaka 2006 hadi 2015 jumla ya matukio 56 ya uhalifu dhidi ya watu
wenye ulemavu wa ngozi yaliripotiwa nchini. Matukio 41 yalihusisha vifo
43, matukio 13 yalihusisha majeruhi 13 na matukio 2 ya kupotea kwa watu
wenye ulemavu wa ngozi” alifafanua Mhe. Silima
“kesi
46 kati ya matukio 56 zilifikishwa Mahakamani ambapo kesi 10 zenye
watuhumiwa 12 zilitolewa hukumu ya kifo na kumi ziko chini ya upelelezi.
Aidha kesi 26 watuhumiwa wake waliachiwa huru kwa kukosa ushahidi”
aliongezea Mhe. Silima
Kuchelewa
kwa hukumu au upelelezi wa baadhi ya kesi zilizotajwa kunachangiwa na
sababu mbalimbali kama vile matokeo ya uchunguzi wa DNA toka Mamlaka ya
Uchunguzi na/au mashahidi kutopatikana kwa urahisi na kwa wakati.
Post a Comment