Jopo maalum limeundwa ilikuwachunguza maafisa wakuu serikalini na wanasiasa ambao wametuhumiwa kuhusika na ufusadi.
Idara
ya kuchunguza masuala ya jinai,tume ya kukabiliana na ufisadi pamoja na
afisi ya mashtaka ya umma zinasema zimekamilisha baadhi ya kesi.
Mashirika
ya kiraia yamekua yakimshinikiza rais Uhuru Kenyatta kuwataja wote
wanaotuhimiwa na ufisadi ambao umesababishia nchi kupoteza mamilioni ya
pesa.
Waziri wa kilimo wa Kenya akiandamana na mawakili kadhaa, aliwasilia katika makao makuu ya tume ya kupambana na ufisadi,
muda mfupi baada ya saa sita za mchana majira ya Afrika Mashariki, huku akiwa kwenye msafara wa magari matatu ya kifahari.
Akiwa amevalia suti ya kijivu, waziri huyo alionekana mchangamfu kinyume na unavyomtarajia kiongozi aliyesimamisha kazi.
Kabla ya kuingia ndani aliwafahamisha waandishi wa habari kuwa hana lolote hadi atakapomaliza.
Dakika
arubaini na tano baadaye, Kosgei alijitokeza tena na kusema kuwa
ameshauriana na mmoja wa wakurugenzi wa tume hiyo, na kinyume na
alivyotarajia,
alifahamishwa kuwa kwa sasa tume hiyo haina nyaraka
zozote za kuonyesha sababu zilizopelekea jina lake kuorodheshwa
miongoni mwa washukiwa wa ufisadi. Kupitia kwa mawakili wake Kosgei
alikuwa ametaka tume hiyo kumweleza madai dhidi yake,
orodha ya
walalamishi, nyaraka zilizowasilishwa mbele ya tume hiyo na walalamishi
au stakabadhi zozote kuhusiana na madai yanayomkabili.
Waziri huyo aliyesimamisha kazi itabidi asuburi hadi siku ya alhamisi wiki hii.
Mawaziri watano na maafisa
wengine wengi wa taasisi za umma wamesimamishwa kazi kwa muda kuhusiana
na madai ya kuhusika na ufisadi.
Akilihutubia bunge la Kenya wiki
iliyopita, rais Uhuru Kenyatta aliagiza maafisa wote wakuu serikalini
waliotajwa na tume ya kupambana na ufisadi
kungatuka madarakani kwa muda wa siku sitini ili kuruhusu uchunguzi wa kina.
Kwingineko, jopo maalum limeundwa ili kuchunguza madai dhidi ya mawaziri hao na maafisa wakuu serikaini,
ambo
wamesimamishwa kazi nchini Kenya kuambatana na agizo la rais Kenyatta,
kuwa maafisa hao wana siku sitini kukamilisha uchunguzi huo.
Jopo hilo litajumuisha maafisa kutoka idara ya mashtaka ya umma, tume ya kupambana na ufisadi na idara ya ujasusi.
Wakati huo huo maafisa wa kaunti ya nairobi leo walinasa punda watano waliokuwa wamefungwa na minyororo kati kati mwa mji mkuu.
Punda hao walikuwa wamepakwa rangi nyekundu na maandishi yanayopinga ufisadi.
Punda mmoja alikuwa na maandishi ya kimombo ''Corruption bleeding Kenya dry'' yaani Ufisadi unamaliza taifa la Kenya
Punda
mwingine naye alikuwa na maandishi mengine mgongoni inayowakejeli
baadhi ya wabunge wa Kenya ambao wametuhumiwa kuhusika na unyanyazaji wa
kimapenzi.(BBC)
Post a Comment