Japan yatoa Sh27 bilioni kusaidia kupunguza foleni Dar

Dodoma. Serikali ya Japan imetoa kiasi cha Sh27 bn kwa Tanzania ili kufanikisha ujenzi wa barabara za juu (Fly-Over) katika eneo la Ubungo, jijini Dar es Salaam.
Hata hivyo kiasi kinachohitajika ni Sh78 bn ili kujenga barabara za juu kutoka Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) hadi katikati ya mji.
Hayo yamesemwa leo la Waziri wa Ujenzi, Dk John Magufuli mjini Dodoma alipokuwa alipokuwa akijibu swali la nyongeza la Mbunge wa Viti Maalum, Rita Mlaki (CCM).
Dk.  Magufuli alisema Serikali ina nia ya dhati ya kupunguza msongamano wa magari kwa Jiji la Dar es Salaam ndio maana inajenga Fly Over katika barabara mbalimbali za jiji hilo.
Katika swali la msingi la msingi, Mbunge wa Viti Maalum, Mariam Kisangi (CCM),  alitaka kujua mpango wa serikali wa kuendeleza mji wa Kigamboni.
Pia alihoji mpango wa serikali wa kujenga kiwanja cha ndege katika mji huo wa Kigamboni.
Akijibu, Naibu Waziri wa Uchukuzi, Chalres Tizeba, alisema serikali inayo mipango ya kuendeleza Mji wa Kigamboni chini ya Usimamizi wa Mamlaka ya Uendeshaji wa Mji wa huo. Tizeba alisema mji huo umo ndani ya Jiji la Dar es Salaam ambako JNIA kipo.
“Kiwanja hiki kina uwezo wa kuhudumia ndege zipatazo 30 kwa saa baada ya kukamilika kwa upanuzi wa miundombinu na ukarabati wa awamu ya pili uliofanyika kati ya mwaka 2008 na 2011,” alisema.
Alisema kwa sasa kiwanja kinahudumia wastani wa ndege nane kwa saa ambazo ni chini ya wastani.
Alisema mpango uliopo ni wa kupanua JNIA kwa kujenga jengo jipya la tatu la abiria

Post a Comment

أحدث أقدم