Wanawake
wote walioamua kupamba sehemu zao za siri kwa kuzitoboa wanachukuliwa
kuwa wamepitia ukatili wa kijinsia ama wamekeketwa kitengo cha afya
kimetanabahisha hayo.
Hata kama mtu huyo amefikia umri wa utu
uzima na ameyafanya hayo kwa ridhaa yake,bado atahesabika kuwa alipitia
ukatili wenye madhara kwa afya yake,na inapaswa kuchukua tahadhari kubwa
kuweka kumbu kumbu za watu walio toboa sehemu zao za siri.
Lakini
kujichora mwilini maarufu kama Tattoo ama kutoboa sehemu za siri ama
mwilini,kumepingwa na taasisi ya utoboaji na uchoraji tattoo mwilini
kwamba hakuna uhusiano wowote na ukeketaji.
Na kueleza kuwa vitu
hivyo viwili havichangamani kulinganisha na kutoboa sehemu za mwili wa
mwanadamu,na taasisi hiyo wanachukulia suala la kutoboa mwili kama jambo
la kaiwada na la ridhaa anasema msemaji wa taasisi hiyo Marcus
Henderson.
Zaidi ya matukio ya ukeketaji yapatayo mia mbili
yalichunguzwa na polisi wa kimataifa miaka mitano iliyopita,na
inashauriwa kama kuna mtu mmoja ana mashaka na suala ya ukeketaji
wataarifu polisi.
Watoboaji makini huwa hawataki
kuumiza wateja wao na huwa hawataki kuonesha tundu za kazi zao na hawako
tayari kumtoboa mtu aliye chini ya umri wa miaka kumi na nane,anaeleza
Mr Henderson.
Mtoboaji maarufu kutoka mjini London ambaye ametaka
ahifadhiwe jina lake, amesema kwamba wateja walio wengi huwa wanataka
kutobolewa sehemu zao za siri zisilingane na ukeketaji.
Sihusiki
na ukeketaji,nadhani utoboaji ni zaidi ya pambo mwilini ama uvumbuzi
mpya wa kihisia zaidi.Mtoboaji huyu anadai kwamba huwa anaitekeleza kazi
yake kwa ufanisi mkubwa,kwanza huangalia picha kwa umakini mkubwa kabla
hajamtoboa mtu, na kamwe hawezi kumtoboa mtu aliye na umri wa chini ya
miaka kumi na nane.Na wateja wake walio wengi ni wanawake na hutoboa
sehemu ya siri hasa kwenye pezi la sehemu ya kati ya maungo ya mwanamke.
Ingawa
mtoboaji huyu mashuhuri mwanzoni alikuwa hakubali kutoboa sehemu za
siri za wanawake,na hii ni kutokana na maungo yao yalivyo na hatari
inayowakabili kupitia utaratibu huo.
Naye msemaji kutoka kitengo
cha afya ambaye ni mwanamke anasema kwamba,kuna changamoto kwa baadhi ya
maeneo wanawake watu wazima hutobolewa sehemu zao za siri kilazima na
maeneo mengine wasichana hulazimishwa kutobolewa.
Idadi ya wanawake waliokeketwa
nchini Uingereza inatajwa kufikia laki moja na elfu sabini,na zaidi ya
wanawake na wasichana elfu mbili na mia sita wamehudumiwa na kitabibu
tangu September na kati ya hao ,mia nne tisini na tisa walitambuliwa
January mwaka huu pekee.
Nayo serikali ya Uingereza imesema kwamba
haina mpango wa kuifanyia marekebisho sheria ya mwaka 2003 kuingiza
suala la kufanya upasuaji kwa masuala ya urembo kwenye sehemu za siri.
Kamati
teule ya wabunge katika taarifa yake imesema kwamba sheria hiyo haina
budi kubadilishwa ili kuweka wazi juu ya taratibu hizo kuwa ni kinyume
cha sheria na zaidi ni kosa la jinai kama zitafanywa kwa msichana wa
chini ya miaka kumi na nane isipokuwa kwa sababu ya afya ya akili au
kimwili.
Post a Comment