Mapigano makali yanashuhudiwa nje na ndani ya uwanja wa ndege katika mji wa Aden nchini Yemen.
Taarifa
zinasema maafisa wa polisi waaminifu kwa aliyekuwa rais wa nchi hiyo,
Ali Abdullah Saleh, walishambulia sehemu moja ya uwanja wa ndege, lakini
wakakabiliwa na makundi ya usalama yanayomuunga mkono rais wa sasa,
Abed Rabbo Mansour Hadi.
Milipuko kadhaa imetokea katika uwanja
huo na abiria waliagizwa kushuka kwenye ndege iliyokuwa inatarajiwa
kuondoka kuelekea Cairo.
Washambuliaji watatu waliuwawa katika mapigano huku kumu kati yao wakitiwa mbaroni.
Aden
ni ngome kuu ya rais Abdrabbuh Mansour Hadi, aliyekwepa nyumbani
alikokuwa anazuiliwa katika mji mkuu Sanaa baada ya waasi wa madhehebu
ya kishia - Houthi kulidhibiti kikamilifu eneo hilo mnamo mwezi Januari.(BBC)
Post a Comment