Mkurugenzi
wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC),
Harold Sungusia (kushoto), akizungumza katika mkutano na waandishi wa
habari Dar es Salaam leo asubuhi kwa niaba ya Mkurugenzi Mtendaji wa
kituo hicho, Dk. Helen Kijo-Bisimba, wakati akitoa taarifa juu ya
mwenendo na hatua za kisheria kwa viongozi wa umma wanaokiuka
maadili.Katikati ni Mkurugenzi wa Ujengaji Uwezo na Uwajibikaji wa LHRC,
Imelda Urrio na kulia ni Ofisa Programu Dawati la Waangalizi Watendaji
wa Serikali wa LHRC, Hussein Sengu.
Kituo
cha sheria na haki za binadamu nchini tanzania (LHRC) leo kimeitaka serikali kuwawajibisha
viongozi ambao wamekuwa wakitoa kauli ambazo wamedai kuwa zinaonyesha dharau na
kebehi kwa watanzania kwani kufanya hivyo kutaonyesha uwajibikaji kwa viongozi
wa Tanzania.
Akizungumza
na wanahabari leo jijini Dare s salaam kwa niaba ya mkurugenzi
mtendaji wa kituo cha sheria na haki za binadamu nchini Tanzania,Mkurugenzi wa Utetezi na Maboresho wa Kituo cha Sheria na Haki za Binadamu (LHRC), Harold Sungusia amesema kuwa kauli ambazo zimekuwa zikitolewa na
baadhi ya viongozi wa serikali kwa wananchi wao zimekuwa zikionyesha dharau na
kebehi kwa watanzania na ni hali inayoonyesha kumomonyoka kwa maadili miongoni
mwa viongozi wa Tanzania.
Amesema kuwa kumekuwa na kauli za dharau na kejeli
ambazo zimekuwa zikitolewa kwa wananchi kutoka kwa viongozi wao pale ambapo
wananchi wanapohoji mambo ya msingi na
kumekuwa hakuna hatua zozote ambazo zimekuwa zikichukuliwa kwa viongozi hao
jambo ambalo amesema kuwa linawapa kiburi kuwa hakuna yoyote anayeweza kuhoji.
Wanahabari wakichukua taarifa hiyo.
Akitolewa mfano wa baadhi ya kauli ambazo zimewahi
kutolewa na viongozi wa Tanzania amesema kuwa moja ya kauli ya kuudhi
iliyotolewa katika sakata la pesa za ESCROW ambayo ilitolewa na aliyekuwa
waziri wa ardhi ANNA TIBAIJUKA ambapo wakati akihojiwa na baraza la maadili alisema kuwa “HIYO MILLION KUMI SI
NI PESA YA MBOGA TU”kauli ambayo amesema kuwa inaudhi ukizingatia kuwa
watanzania wengi wanaishi chini ya dola moja.
Kauli nyingine zilizotolewa na viongozi mbalimbali
wakati wakijitetea katika ukwapuaji wa fedha za ESCROW ni pamoja na “SIKUMWOMBA
JAMES RUGEMALILA ANIWEKEE HELA,NA SIJUI KWA NINI ALINIWEKEA HELA HIZO,HATA
ALIVYONIAMBIA NIFUNGUE ACCOUNT BANK YA MKOMBOZI ILI ANIWEKEE FEDHA HIZO
SIKUMUULIZA FEDHA HIZO NI ZA NINI”
Kauli nyingine ni ile inayosema “NINA ACCOUNT NYINGI
NA ZA NJE YA NCHI NINGETAKA NINGEMWAMBIA AZIWEKE FEDHA ACOUNT ZA HUKO”.
Amesema kuwa kauli hizo zilizotolewa katika sakata
la kuwahoji wahusika wa ukwapuaji wa fedha za ESCROW ni mwendelezo wa kauli ambazo
zimewahi kutolewa na viongozi kipindi cha nyuma kama kauli aliyowahi kuitoa
waziri CHENGE KUWA “hivi ni vijisent tu”na ile ambayo aliitoa waziri MAGUFULI
ya kuwataka wananchi wa kigamboni kama watashindwa kulipa mia mbili ya kuvuka
na panton bora waogelee kauli ambayo iliwaacha baadhi ya watanzania midomo wazi
kwa kusikia kauli kama hivyo kwa kiongozi waliyemchagua.
Amesema kuwa kwa kauli hizo ni wazi kuwa Tanzania
bado ina tatizo kubwa katika katika swala la uongozi na uwajibikaji wa viongozi
katika mfumo mzima wanchi.
Aidha amesema kuwa ili kukabiliana na changamoto hii
ya viongozi wa Tanzania ni lazima sheria ya maadili ya viongozi wa umma
itekelezwe kama ilivyoanishwa na secretarieti ya maadili ya viongozi wa
umma,ikiwa ni pamoja na viongozi kuwajibishwa kwa kauli zao zenye kuonyesha
dharau kwa wananchi wa Tanzania.
Katika hatua nyingine bwana sungusia amesema kuwa ikiwa
Tanzania inaelekea katika mchakato wa kupata katiba mpya lakini bado katiba
iliyopendekezwa kwa ajili ya kupigiwa kura haijashinikiza uwepo wa uwajibikaji
kwa viongozi watakaochaguliwa kwa ajili ya kuwatumikia watanzania hivyo bado
katiba ijayo haiwezi kuwa dawa ya tatizo hilo nchini.
Miaka ya hivi karibuni kumeibuka kauli ambazo
zimekuwa zikitolewa na viongozi wa tanzania ambazo zimekuwa zikionekana kama ni
dharau kwa watanzania jambo ambalo limeanza kupigiwa kelele na wanaharakati
wengi wakidai kuwajibishwa kwa wanaotoa kauli hizo.
إرسال تعليق