Siku ya leo moja ya story kubwa ambayo
ilikuwa ikisambaa kwa kasi mitandaoni na watu ambao hawakuingia
mitandaoni walikutana na ujumbe ambao watu walikuwa wakisambaziana watu
kwamba kuna msiba wa msanii wa kundi la Orijino Komedi, Clouds FM
ikawatafuta Joti pamoja na Seki abao walikanusha juu ya tetesi kwamba
msanii Vengu amefariki.
Ni muda mrefu msanii huyo hajaonekana, timu ya #AMPLIFAYA zilifanya jitihada na kumpata Andrew Shamba ambaye ni kaka wa Joseph Shamba aka Vengu, hapa akaanza kuzungumzia jinsi tetesi hizo walivyozipokea; “Familia
inatusikitsha kwa maana kwamba haina ukweli wowote hii ishu ni zaidi ya
mara tano wanazungumza hao wat.. na hao watu hawazungumzi kwa mapenzi
mazuri Vengu sasa hivi ana hali nzuri vitu vidogo vidogo anajisaidia yeye mwenyewe, hizi habaru za uvumi zinakatisha tamaa..“
“Vengu
sasa hivi ana mwaka mmoja na nusu yuko nyumbani kama anaenda Hospitali
ni binadamu.. labda Malaria, au labda kichwa kitamuuma ndio tutasema
twende Hospitali lakini sio mgonjwa na Komedi wanajua kwamba amepumzika
na wao wamekubali kwamba apumzike ili baadae arudi..“
“Madaktari
wake ni wakali mno kuna daktari wake hataki suala la kufanya mahojiano
au kumkumbusha kumbusha vitu vya nyuma inakuwa kama unamtia huzuni..
kumpa simu asikilize ni vitu ambavyo vimekatazwa“
Ni muda mrefu msanii huyo hajaonekana akiigiza pamoja na kundi lake la Orijino Komedi; “Vengu ameanza kuumwa 2011 mwezi wa tisa“–Andrew Shamba.
Post a Comment