KIUNGO
mshambuliaji wa Simba, Simon Sserunkuma, amesema kuwa hana furaha na
maisha yake kwa sasa ndani ya klabu hiyo na anaomba aruhusiwe atimke.
Kiungo huyo amesema hana furaha kutokana na kuwekwa benchi na kocha Mserbia, Goran Kopunovic.
Nyota huyo aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo msimu huu akitokea Express ya Uganda, amekuwa na maisha magumu kwa sasa kwa kujikuta akikaa benchi kwenye michezo mingi.
Nyota huyo aliyesajiliwa wakati wa dirisha dogo msimu huu akitokea Express ya Uganda, amekuwa na maisha magumu kwa sasa kwa kujikuta akikaa benchi kwenye michezo mingi.
Akizungumza na Championi Jumatano, Sserunkuma ambaye ni ndugu wa Dan
Sserunkuma ambaye ameshatangaza kutimka, amesema kuwa kwa ujumla
hafurahii maisha yake kwa sasa, kwani alikuja kucheza na siyo kuchoma
mahindi, maisha ambayo hajayazoea.
Alikwenda mbali na kusema kuwa bado hajaona timu ambayo inamfaa hapa
Tanzania kupelekwa kwa mkopo, kwa kile alichosema zote ni ndogo, hivyo
angetamani kuangalia mbele zaidi.“Binafsi sina furaha kwa kifupi, kwanza
nilikuja huku kucheza mpira na siyo kukaa benchi na walinihakikishia
hilo wakati nakuja, lakini pia mimi nimechezea katika timu nyingi tena
kubwa, sijawahi kukutana na maisha kama haya.
“Of course’ ni lazima niumie maana nitakuwa najiharibia mwenyewe
kipaji, ni bora nipate sehemu ambayo ninaamini nitapata uhakika wa
kucheza,” alisema kiungo huyo.
إرسال تعليق