Kondomu zaziba mitaro ya maji taka


KAMPUNI  inayoshughulikia maji na majitaka mjini Lusaka, Zambia LWSC imelalamika tabia mbaya  za watu kuflashi kondomu na kusababisha kuziba kwa mitaro ya majitaka mjini humo.
Kampuni hiyo imesema kwamba hivi karibuni imelazimika kuzibua mtaro mitaro ambayo imezibwa na kondomu zaidi ya 1000.
Aidha kampuni hiyo imesema kwamba kila siku wanatoa kondomu 1000 zinazoziba mitaro hali inayotishia usafi wa mji huo.
Ofisa uhusiano wa kampuni hiyo  Topsy Sikalinda  amesema kwamba taasisi yake inafanya juhudi ya  kumtambua mtu ambaye anatupoa kondomu kw anamna ambayo inasababisha tatizo kwa watu wengine kama kuziba kwa mabomba ya kusafirisha uchafu.
Amesema kwamba kampuni hiyo inaliona tatizo hilo kuwa kubwa kutokana na kuzidi na hivyo kuonekana kuhitaji angalizo maalumu.
 “Tunaondoa kondomu 1000 kila siku  ambazo hazikuhifadhiwa inavyotakiwa baada ya matumizi na zinaziba njia zetu za maji machafu. Kuna wakati tunakuta nguo,taulo za kike na hata vipande vya matofali matofali,” alisema Sikalinda.
“Tutaanza kusaka chanzo cha vitendo hivi kuhakikisha kwamba tunawashtaki chini ya sheria ya maji na usafi.”

Post a Comment

Previous Post Next Post