London, England. Wiki iliyopita zilifahamika timu nane ambazo zimeingia hatua ya robo fainali ya Ligi ya Mabingwa Ulaya msimu wa 2014/15.
Timu hizo nane ni Real Madrid, Bayern Munich, Paris Saint-Germain, Porto, Barcelona, Atletico Madrid, Monaco na Juventus.
Tayari ratiba ya mechi za robo fainali imepangwa
huku mechi za kwanza za hatua hii zikipangwa kuchezwa Aprili 14 na 15
wakati mechi za marudiano zitachezwa Aprili 21 na 22, 2015.
Ratiba hiyo inaonyesha Paris Saint-Germain
itakipiga na Barcelona huku Atletico Madrid ikikipiga na Real Madrid
wakati Porto itakuwa na kibarua kigumu kwa Bayern Munich, pia Juventus
itakipiga na Monaco.
Mpaka sasa katika mashindano hayo ya Ligi ya
Mabingwa Ulaya, mshambuliaji wa Shakhtar Donetsk, Luiz Adriano ambaye
timu yake ilitolewa katika hatua ya 16 bora ya mashindano hayo ndiye
anayeoongoza chati ya ufungaji akiwa na mabao tisa akifuatiwa na Lionel
Messi (Barcelona) na Cristiano Ronaldo (Real Madrid) ambao wana mabao
nane kila mmoja.
Messi na Ronaldo ambao wanakipiga katika Ligi Kuu
ya Hispania (La Liga), timu zao bado zipo katika mashindano ya Ligi ya
Mabingwa hivyo mmojawapo anapewa nafasi kubwa ya kuwa mfungaji bora
katika mashindano hayo.
Nyota hawa wamekuwa wakishindana katika kuwania
tuzo ya mchezaji bora wa dunia (Ballon d’Or) huku Messi akiitwaa mara
nne na Ronaldo mara tatu, pia wamekuwa wakishindana katika kuwania tuzo
ya mfungaji bora wa La Liga (Tuzo ya Pichichi).
Hivi sasa Ligi ya La Liga inaendelea huku Messi
akiwa anaongoza kwa kufunga mabao akiwa nayo 32 akifuatiwa na Ronaldo
mwenye mabao 31.
Pia, Ronaldo na Messi wameishavunja rekodi ya
kufunga mabao 50 kwa msimu na kila mmoja ameishafunga zaidi ya mabao 400
katika mechi walizochezea klabu zao na timu za taifa.
Kutokana na rekodi walizonazo,je, ni Messi au
Ronaldo atakayeibuka kuwa mfungaji bora wa Ligi ya mabingwa Ulaya? au
watakuwa Karim Benzema (Real Madrid), Carlos Tevez (Juventus) na Edinson
Cavani (Paris Saint-Germain) wenye mabao 6 katika mechi za ligi hiyo?
Vita ya Messi, Ronaldo yanoga
إرسال تعليق